Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Syria: Askari wa Uturuki auawa, wanne wajeruhiwa Idlib

Askari mmoja wa Uturuki ameiuawa na wengine wanne wamejeruhiwa katika mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria katika shambulio la roketi dhidi ya msafara wa chakula kwa wanajeshi, wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema.

Wanajeshi wa jeshi la Uturuki katika mji wa Binnish kaskazini magharibi mwa mkoa wa Idlib Februari 12, 2020.
Wanajeshi wa jeshi la Uturuki katika mji wa Binnish kaskazini magharibi mwa mkoa wa Idlib Februari 12, 2020. Muhammad HAJ KADOUR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Uturuki vigundua eneo ambako shambulio lilikuwa ylikitokea na kujibu kwa kulipiza kisasi, taarifa ya wizara imesema. Haikusema aliyehusika na shambulio hilo.

Hayo yanajiri wakati Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki anaitembelea Saudi Arabia kwa mara ya kwanza tangu mauaji ya mwandishi mkosoaji wa Saudi Arabia, Jamal Khashoogi 2018, yalipouharibu uhusiano wa nchi hizo, ambao toka hapo ulikuwa wa mashaka.

Mevlut Cavusoglu yuko mjini Riyadh tangu jana Jumatatu na kleo Jumanne ambapo atakutana na mwenzake Faisal bin Farhan na kujadili masuala ya uhusiano baina ya mataifa yao pamoja na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kikanda.

Ziara hiyo ya Cavusoglu inafanyika baada ya wiki iliyopita kufanyika mkutano wa manaibu mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na Misri uliolenga kutatua mivutano ya muda mrefu baina ya mahasimu hao wa kikanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.