Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Tofauti zaibuka kati ya Tripoli na Uturuki juu ya uwepo wa vikosi vya kigeni

Mawaziri wa Mambo ya nje na Ulinzi wa Uturuki walikuwa mjini Tripoli Jumatatu, Mei 3, kwa ziara nyingine. Walikutana na maafisa wakuu wa serikali ya mpito nchini Libya. Tofauti ziliibuka katika taarifa kutoka pande mbili kuhusu mamluki walioko nchini humo. Maafisa kutoka nchi hizi mbili  hawazungumzi kwa kauli moja kuhusu suala hili.

Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu akutana na Waziri Mkuu wa Libya Abdel Hamid Dbeibah huko Tripoli, Libya mnamo Mei 3, 2021.
Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu akutana na Waziri Mkuu wa Libya Abdel Hamid Dbeibah huko Tripoli, Libya mnamo Mei 3, 2021. VIA REUTERS - Media Office of the Prime Minist
Matangazo ya kibiashara

"Tunatoa wito kwa Uturuki kushirikiana nasi kumaliza uwepo wa vikosi vyote vya kigeni na mamluki ili kulinda uhuru wetu," amesema Najla Mangoush, Waziri wa Mambo ya nje wa Libya, katika mkutano wa pamoja na mwenzake wa Uturuki. Kwa upande wake, Waziri wa mambo yaje wa Uturuki amekosoa "kauli hizo ambazo zinalinganisha uwepo wa Uturuki nchini Libya na kuwepo kwa makundi mengine haramu".

Mnamo mwaka 2019 Ankara ilisaini mkataba wa kijeshi na serikali ya Sarraj, kisha ikatuma maelfu ya mamluki wa Syria na zaidi ya wanajeshi na maafisa wake nchini Libya. Leo, Uturuki haionekani kuwa na haraka kuondoka katika nchi hii na kila wakati inakumbusha msimamo wake wa mara kwa mara: uwepo wa vikosi vyake umezuia Libya "kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe".

Kuondoka kwa mamluki ni moja wapo ya changamoto kubwa ya serikali ya mpito nchini Libya. Jan Kubis, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, aamekuwa anasisitiza juu ya haja ya kuondoka kwa mamluki katika kila mkutano na afisa wa Libya. Tangu mkataba wa kusitisha mapigano, hali ya usalama inaendelea kudorora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.