Pata taarifa kuu
UTURUKI

Uturuki yaidhinisha matumizi ya dharura ya chanjo ya Sputnik V

Shirika la Dawa la Uturuki leo Ijumaa limeidhinisha utumiaji wa dharura wa chanjo ya Sputnik V dhidi ya COVID-19.

Virusi vya Corona ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu.
Virusi vya Corona ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. REUTERS - UMIT BEKTAS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano Ankara ilitangaza kutiwa saini kwa mkataba wa kusambaza dozi milioni 50 za chanjo ya Urusi kwa kipindi cha miezi sita. Chanjo ya kwanza inatarajiwa mwezi ujao.

Chanjo mbili hadi sasa zimeidhinishwa nchini Uturuki, ile ya maabara ya Marekani ya Pfizer na mshirika wake BioNTech kutoka Ujerumani na ile ya maabara ya China Sinovac Biotech.

Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.

Virusi vya Corona vya COVID-19 ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. Dalili zake ni pamoja na homa, kikohozi, shida katika kupumua, na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha, nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanyakazi kwa figo na hata kifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.