Pata taarifa kuu
UTURUKI-CORONA-AFYA

Waandamanaji kadhaa wakamatwa na polisi Uturuki

Polisi ya Uturuki imewakamata viongozi kadhaa wa vyama vya wafanyakazi walio kuwa wanaandamana leo Ijumaa Mei 1 huko Istanbul kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani licha ya marufuku ya kutotembea yaliyowekwa kwa lengo la kudhibiti janga la Covid-19.

Hivi karibuni Waziri wa Afya Fahrettin Koca, aliwasihi wananchi wa Uturuki waendelee kufuata sheria ya kukaa ndani kwani imezaa matunda.
Hivi karibuni Waziri wa Afya Fahrettin Koca, aliwasihi wananchi wa Uturuki waendelee kufuata sheria ya kukaa ndani kwani imezaa matunda. REUTERS/Dado Ruvic
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu kumi na tano, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa shirikisho kuu la vyama vya wafanyakazi DiISK, Arzu Cerkezoglu, wamekamatwa na polisi, amebaini mpiga picha wa shirika la habari la AFP.

Hivi karibuni Waziri wa Afya Fahrettin Koca, aliwasihi wananchi wa Uturuki waendelee kufuata sheria ya kukaa ndani kwani imezaa matunda.

Idadi ya wagonjwa waliopona ugonjwa wa Covid-19 iliogezeka kwa kasi nchini Uturuki wiki hii

Kulingana na Waziri wa Afya wa nchi hiyo,idadi ya waliopona imezidi idadi ya kesi mpya za maambukizi.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Fahrettin Koca, waziri wa afya wa Uturuki alisema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imefikia zaidi ya 3,845, huku kesi mpya za maambukizi zikiwa ni 2861 hadi aprili 26.

Siku ya Wafanyakazi inasherehekea leo Ijumaa duniani kote wakati ambapo nchi nyingi zinaendelea kukumbwa na janga la Covid-19, huku masharti ya watu kutotembea yakiendelea kutekelezwa katika nchini nyingi duniani, licha ya nchi kadhaa hususan, zile za Ulaya, na Marekani na baadhi ya nchi za Afrika ziliitangaza kuanza kulegeza vizuizi hivyo.

Virusi hivi vilianzia China mnamo mwezi Desemba mwaka jana na mpaka sasa vimeenea na kuathiri nchi zaidi ya 185 duniani.
Kulingana na takwmimu zilizojumuishwa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani, mlipuko huo umewauwa watu zaidi ya 200,000, na kuambukiza jumla ya zaidi ya milioni 2.84, wakati zaidi ya 803,000 wakiwa wamepona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.