Pata taarifa kuu
UTURUKI-LIBYA-USALAMA-USHIRIKIANO

Afisa wa idara ya ujasusi wa Uturuki auawa nchini Libya

Habari hii ilianza kusambaa baada ya siku kadhaa za sintofahamu. Taarifa hii ilianza kusambaa wakati wapiganaji wa kundi la ANL la Marshal Khalifa Haftar walidai kuwa waliwauwa askari 16 wa Uturuki katika mashambulizi ambayo yalilenga bandari ya mji mkuu, Februari 18.

Kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Fayez el-Sarraj (kushoto) alisaini makubaliano ya kijeshi na Rais Recep Tayyip Erdogan nchini Uturuki, Istanbul, Novemba 27, 2019.
Kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Fayez el-Sarraj (kushoto) alisaini makubaliano ya kijeshi na Rais Recep Tayyip Erdogan nchini Uturuki, Istanbul, Novemba 27, 2019. Mustafa Kamaci / TURKISH PRESIDENTIAL PRESS SERVICE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi iliyopita, rais wa Uturuki Reçep Tayyip Erdogan alikubali kuwapoteza askari wake kadhaa nchini Libya na hapo alikiri kifo cha askari wawili, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu tarehe wala mahali.

Leo, habari mpya zimepelekea kutambua afisa wa idara ya ujasusi wa Uturuki, MIT, Kanali Okan Altinay kwamba aliuawa nchini Libya.

Alizaliwa mnamo mwaka 1971, alikuwa anasimamia zoezi la kutoa silaha kutoka Uturuki kwenda Tripoli, makao makuu ya serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa na jumuiya ay kimataifa.

Kulingana na wapiganaji wa ANL, Kanali huyo, ambaye kawaida alikuwa akiishi katika eneo la jeshi la uwanja wa ndege wa Matigua, alienda bandarini kupokea silaha.

"Tulifanya shambulio bandarini, kufuatia habari sahihi tulioipata," Ahmad al-Mismari, msemaji wa wapiganaji wa ANL wanaoongozwa na Marshal Khalifa Haftar amesema.

Miili ya askari hao wawili ilisafirishwa kwa siri kubwa nchini Uturuki kwa kutumia ndege ya kiraia ya Libya usiku wa Februari 18. Katika siku za hivi karibuni, vyombo vya habari vya Uturuki vimesema, vikinukuu familia na ndugu wa Kanali Okan Altinay, kwamba alizikwa kwa siri, bila sherehe ya kijeshi katika kijiji chake katika mkoa wa Aydin, magharibi mwa Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.