Pata taarifa kuu
LIBYA-ALGERIA-UPATANISHI-USALAMA

Algiers yapendekeza kuwa mpatanishi katika mgogoro wa Libya

Katika mahojiano na gazeti la Le Figaro yaliyochapishwa Alhamisi wiki hii, rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amependekeza nchi yake kuwa mpatanishi katika mgogoro ambao unaendelea nchini Libya.

Licha ya makubaliano ya kimataifa kutangazwa huko Berlin, mapigano bado yanaendelea.
Licha ya makubaliano ya kimataifa kutangazwa huko Berlin, mapigano bado yanaendelea. Mahmud TURKIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo rias Abdelmadjid Tebboune amefutilia mbali kuwa nchi yake inatafuta "maslahi" au inalenga utajiri wa nchi hii iliyogawanika mara mbili tangu kuangika kwa utawala wa Mouammar Gaddafi mwaka 2011.

"Leo, lazima tuwalazimishe Walibya kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kujenga tena taifa lao," rais Tebboune, aliyechaguliwa mwezi Desemba mwaka jana, amesema katika mahojiano hayo.

"Ikiwa tutapewa nguvu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, tunaweza kuleta amani haraka nchini Libya kwa sababu Algeria haina upande inayoegemea kwa pande hasimu nchini Libya na inakubaliwa na pande zote hizo zinazokinzana nchini Libya, " amebaini rais Tebboune

"Libya ina bahati kubwa kwa sasa kutokana na kwamba makabila yake makubwa hayakuchukua silaha" na "wote wako tayari kuja Algeria kujenga mustakabali wa pamoja", ameongeza rais wa Algeria. "Sisi pekee ndio tunapendekeza suluhisho zinazojenga. Hatujaachwa kufanya. Lakini, Algeria haina lengo lolote la kimaslahi kwa utajiri wa nchi hii ndugu, " amesema rais Tebboune.

Libya ambayo ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2011,imegawanywa katika kambi mbili za hasimu, kati ya serikali ya kitaifa (GEN) inayoongozwa na Fayez al Sarraj, ambayo makao yake makuu ni Tripoli na ambayo inatambuliwa na jamii ya kimataifa, na serikali inayoungwa mkono na Marshal Khalifa Haftar, mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.