Pata taarifa kuu
UTURUKI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Watu 100 wafariki dunia ndani ya saa 24 nchini Uturuki

Karibu vifo vipya mia moja vimeripotiwa ndani ya masaa 24 siku ya Jumapili nchini Uturuki, na kusababisha jumla ya vifo vinahuvyosiana na ugonjwa wa Covid19 kufikia hadi 1,198 nchini, Waziri wa Afya wa Uturuki, Fahrettin Koca ametangaza.

Mji wa Istanbul na wilaya ya Karaköy, Uturuki, Februari 26, 2020.
Mji wa Istanbul na wilaya ya Karaköy, Uturuki, Februari 26, 2020. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Mbali na vifo vipya 97, kesi 4,789 za mpya za maaambukizi mapya za virusi hivi, ambayo ilitokea nchini China mwezi Desemba kabla ya kusambaa hadi nchi mbalimbali duniani, zilibainika ndani ya siku moja, na kiufanya idadi ya wagonjwa kufikia 56,956 tangu kuanza kwa janaga hilo, ameongeza kwenye akaunti yake ya Twitter.

Katika juhudi za kupambana na virusi vya Corona, Uturuki kwa mara ya kwanza ilitangaza marufuku ya kutoka nje mwishoni mwa juma hili.

Hivi karibuni Uturuki ilichukua hatua kali za kuhakikisha usalama na kukabiliana na janga la virusi vya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.