Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Pyongyang yaionya Marekani kuepuka kueneza mtafaruku

Kim Yo-jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, amekosoa mazoezi ya kijeshi yanayoendelea hivi sasa nchini Korea Kusini na kuonya utawala mpya nchini Marekani kwamba haupaswi kueneza mtafaruku ikiwa unataka amani, vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini vimebaini.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na dada yake, Kim Yo-jong, Aprili 27, 2018, kando ya mkutano na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na dada yake, Kim Yo-jong, Aprili 27, 2018, kando ya mkutano na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in. Korea Summit Press Pool/Pool via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii, iliyorushwa na shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA, inakuja siku moja baada ya kuwasili jijini Seoul kwa wawakilishi wakuu wa utawala wa rais wa Marekani Joe Biden kwa mazungumzo ya awali na wenzao wa Korea Kusini.

 

"Tunachukua fursa hii kuonya utawala mpya wa Marekani mbao unajaribu kuleta mtafaruku katika eneo letu," amesema Kim Yo-jong, kulingana na taarifa zilizoripotiwa na KCNA. "Ikiwa anataka amani kwa miaka minne ijayo, bora angeepuka kusababisha ,tafaruku kama hatua ya kwanza."

Siku ya Jumatatu Washington ilisema kwamba ilijaribu bila mafanikio kuwasiliana na Pyongyang "kuzuia wasiwasi unaoendelea kujitokeza", maafisa wamesema.

Marekani na Korea Kaskazini wakabiliwa na uhasama za ndani

Marekani na Korea Kaskazini bado zina hitilafiana juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini na ule wa utengenezaji makombora.

Mikutano mitatu kati ya mtangulizi wa Bwana Biden na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jonh-un ilifikia machache tu.

Donald Trump alikutana na Kim Jong-un mara tatu na kubadilishana barua naye, lakini Korea Kaskazini ilimaliza mazungumzo hayo kwa kutaka Marekani kwanza iachane na sera yake ya uhasama dhidi yake.

Vikosi vya Korea Kusini na Marekani vimeanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwa idadi ndogo ya wanajeshi kutokana na kukabiliana na janga la Corona kama sehemu ya juhudi za mazungumzo na Korea Kaskazini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.