Pata taarifa kuu
MAREKANI-JAPANI

Marekani yataka uhusiano wa karibu na Japan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa kuimarishwa kwa uhusiano wa kiuchumi kati ya Marekani na Japani, kwani anatarajia kutumia fursa ya ziara yake ya kwanza ya kimataifa ya kuimarisha miungano ya Asia ili kuunda ngome yenye nguvu dhidi ya utawala wa China.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na Waziri wa Mambo ya Nje  Antony Blinken wakiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Toshimitsu Motegi na Waziri wa Ulinzi Nobuo Kishi, huko Tokyo, Japan , Machi 16, 2021.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken wakiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Toshimitsu Motegi na Waziri wa Ulinzi Nobuo Kishi, huko Tokyo, Japan , Machi 16, 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani huko Tokyo na Seoul, akiambatana na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin, ni ziara ya kwanza nje ya nchi ya maafisa wakuu wa utawala wa rais Joe Biden na inakuja baada ya mkutano wa "Quad" (mazungumzo kuhusu usalama yaliyojumuisha pande zote kati ya viongozi wa Marekani, Japani, Australia na India).

Miongoni mwa mada ambazo zitajadiliwa Tokyo ni uhuru wa kusafiri katika Bahari ya Kusini ya China, usalama kqtikq eneo hiilo, na suala la nguvu ya nyuklia ya Korea Kaskazini na mapinduzi ya jeshi huko Myanmar.

Akiongea na viongozi wa biashara, Antony Blinken alisema uhusiano wa kiuchumi kati ya Marekani na Japani ni "moja ya nguvu zaidi ulimwenguni," na kuongeza kuwa nchi hizo mbili lazima zishirikiane kwa kuweka nguvu pamoja kwa kuimarisha usalama zaidi katika  siku za usoni.

Marekani na Japani kuijadili Korea Kaskazini

Korea Kaskazini inatarajiwa kuwa miongoni mwa mada itakayojadiliwa wiki hii baada ya Ikulu ya White House kusema ilijaribu kuwasiliana na Pyongyang bila mafanikio, wakati ambapo Korea Kaskazini imeionya Marekani kutosababisha mtafaruku ikiwa inataka amani.

Marekani na Korea Kaskazini bado zina hitilafiana juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini na ule wa utengenezaji makombora.

Mikutano mitatu kati ya mtangulizi wa Bwana Biden na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jonh-un ilifikia machache tu.

Mazungumzo yalishindwa kuishawishi Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia - hitaji la msingi kwa Marekani na nchi zingine za Magharibi zenye nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.