Pata taarifa kuu
ARMENIA-AZERBAIJAN-UTURUKI-USALAMA

Nagorno-Karabakh: Uturuki yaahidi kusaidia Azerbaijan kijeshi ikiwa itaiomba

Uturuki "itafanya kilio chini ya uwezo wake" ikiwa Azerbaijan itaomba msaada wa kijeshi katika mzozo kati yake na Armenia huko Nagorno-Karabakh, Waziri wa Mambo ya nje Mevlut Cavusoglu amesema leo Jumatano.

Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu huko Jeddah, Saudi Arabia, Mei 29, 2019.
Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu huko Jeddah, Saudi Arabia, Mei 29, 2019. REUTERS/Waleed Ali/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizitaja taarifa za Uturuki kuhusu mzozo huo kuwa za " kijinga" na "hatari".

Tangu Jumapili, mapigano yamegharimu maisha ya watu wengi katika eneo hili lililojitenga la Azebaijan, ambalo lina watu wengi kutoka jamii Armenia.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito Jumanne jioni huko New York wa "kusitishwa kwa mapigano". Wanadiplomasia wanajua kuwa huu ni uwanja mwingine wa mapigano kati ya Uturuki na Urusi, kupitia washirika wao.

Haya ndio mapigano mabaya zaidi kuhusu kuwania jimbo hilo tangu mwaka 2016 na ripoti zinasema kuwa vifo vya raia na wanajeshi kutoka pande zote, vimeripotiwa.

Mataifa mbalimbali duniani, yakiongozwa na Marekani, Urusi, Iran na Mataifa ya Ulaya, yametaka pande zote mbili kuacha makabiliano na kuanza mazungumzo.

Tangu mwaka 1991, nchi hizo mbili zimekuwa zikipambania jimbo la Nagorno-Karabakh lililojitangazia uhuru wake kutoka ka Umoja wa Kisoviet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.