Pata taarifa kuu
ARMENIA-AZERBAIJAN-USALAMA

Umoja wa Mataifa watoa wito wa kusitishwa kwa mapigano Nagorno-Karabakh

Tangu Jumapili, vikosi vya wanaharakati wanataka kujitenga wa Nagorno-Karabakh wa kisaidiwa na jeshi la armenia na vile vya Azerbaijan vinakabiliana katika mapigano mabaya zaidi tangu mwaka 2016.

Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh, Septemba 28, 2020.
Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh, Septemba 28, 2020. KAREN MINASYAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito Jumanne jioni huko New York wa "kusitishwa kwa mapigano". Wanadiplomasia wanajua kuwa huu ni uwanja mwingine wa mapigano kati ya Uturuki na Urusi, kupitia washirika wao.

Haya ndio mapigano mabaya zaidi kuhusu kuwania jimbo hilo tangu mwaka 2016 na ripoti zinasema kuwa vifo vya raia na wanajeshi kutoka pande zote, vimeripotiwa.

Mataifa mbalimbali duniani, yakiongozwa na Marekani, Urusi, Iran na Mataifa ya Ulaya, yametaka pande zote mbili kuacha makabiliano na kuanza mazungumzo.

Tangu mwaka 1991, nchi hizo mbili zimekuwa zikipambania jimbo la Nagorno-Karabakh lililojitangazia uhuru wake kutoka ka Umoja wa Kisoviet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.