Pata taarifa kuu
BELARUS-MAANDAMANO-SIASA-USALAMA

Belarus: Umati wa watu waandamana Minsk, watu 400 wakamatwa

Maelfu ya watu wanaandamana jijini Minsk na miji mingine nchini Belarus, katika mwendelezo ya maandamano dhidi ya rais Alexander Lukashenko.

Wabelarus kwa mara nyingine tena wameandamana dhidi ya kuchaguliwa tena kwa rais Alexander Lukashenko Jumapili, Septemba 13, 2020.
Wabelarus kwa mara nyingine tena wameandamana dhidi ya kuchaguliwa tena kwa rais Alexander Lukashenko Jumapili, Septemba 13, 2020. TUT.BY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya maafisa wa polisi wameonekana wakijaribu kuwazuaia waandamanaji hao huku watu zaidi ya 200 wakikamatwa hata kabla ya kuanza kwa maandamano hayo.Maandamano hayo yamekuwa yakishuhudia tangu mwezi uliopita, baada ya Uchaguzi Mkuu ambao wapinzani wanasema uliibiwa na hivyo wanamtaka rais Lukashenko ajiuzulu.

Svetlana Tikhanovskaya, mgombea urais aliyedai ushindi dhidi ya Alexander Lukashenko, na ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Lithuania, katika video, alipongeza "watu mashujaa wa kweli" ambao wanaendelea na "kupigania uhuru".

Licha ya ukubwa wa maandamano hayo, Alexander Lukashenko, aliyeko madarakani tangu 1994, amefuta maelewano yoyote muhimu, akiangazia kufanyamageuzi ya wazi ya Katiba ijayo. Anashutumu mataifa ya Magharibi kuunga mkono maandamano hayo, akiipongeza Moscow kwa msimamo wake baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya nchi hizi mbili.

Mkutano kati ya rais wa Belarus na Vladimir Putin unatarajiwa kufanyika Jumatatu hii Septemba 14.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.