Pata taarifa kuu
BELARUS-MAANDAMANO-SIASA-USALAMA

Maandamano ya kumtaka rais Alexander Lukashenko ajiuzulu yaendelea Belarus

Maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakipambana na polisi wa kupambana na ghasia  jijini Minsk na miji mingine nchini Belarus, kuendelea kushinikiza kujiuzulu kwa rais Alexander Lukashenko.

Belarus yaendelea kukumbwa na maandamano.
Belarus yaendelea kukumbwa na maandamano. Sergei GAPON / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waaandamanaji zaidi 100 wamekamatwa, huku wakiwa karibu na Ikulu ya rais.

Kwa karibu mwezi mmoja sasa, raia wa Belarus wamekuwa wakiandamana kushinikiza Alexander Lukashenko kuondoka madarakani baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliopita ambao mpinzani wake, Svetlana Tikanovskaya alidai kushinda.

Hapo jana pekee, zaidi ya watu laki moja kutoka maeneo tofauti ya nchi hiyo walishiriki katika maandamano hayo licha ya polisi wa kuzuia ghasia kusambazwa katika mji mkuu wa Minsk.

Maandamano hayo hata hivyo yalipelekea kukamatwa kwa watu 250, watu 175 wakikamatwa katika mji mkuu wa Minsk kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Viasna.

Hadi kufikia sasa, maelfu ya wanandamanaji wamezuiliwa na polisi, na wengi kadhaa wamefariki, wengi wao wakiwatuhumu polisi kwa kuwapiga na kuwadhulumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.