Pata taarifa kuu
BELARUS-SIASA-USALAMA

Belarus: Maria Kolesnikova, mmoja wa vigogo wa upinzani, akamatwa mpakani na Ukraine

Kiongozi wa maandamano nchini Belarus Maria Kalesnikava amekamatwa na watu wasiojulikana kwenye mpaka na nchi ya Ukraine. N kufikia sasa hakuna aliyefanikiwa kuwasiliana na Kalesnikava.

Svetlana Tikhanovskaya na Maria Kolesnikova, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii, Agosti 10. S. Tikhanovskaïa, kiongozi mkuu wa upinzani, anamuomba rais anayemaliza muda wake A. Loukachenko, aliyechaguliwa tena rasmi, 'kuachia madaraka'.
Svetlana Tikhanovskaya na Maria Kolesnikova, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii, Agosti 10. S. Tikhanovskaïa, kiongozi mkuu wa upinzani, anamuomba rais anayemaliza muda wake A. Loukachenko, aliyechaguliwa tena rasmi, 'kuachia madaraka'. Sergei GAPON / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa ambazo zimebaini kwamba Maria Kalesnikava ametekwa na watu wasiojulikana katikati ya mji mkuu Minsk na kumpakiza kwenye gari na kuondoka naye, kulingana na shirika la habari la Tut.By la Belarus.

"Kolesnikova kwa sasa anazuiliwa," msemaji wa kikosi cha walinzi wa mpika Anton Bychkovsky ameliambia shirika la habari la AFP juu ya mpinzani huyu ambaye alikuwa wa mwisho kati ya vigogo wanawake watatu katika kampeni ya kupinga rais Alexander Lukashenko kuwania katika uchaguzi a urais ambaye alikuwa bado nchini Belarus. Wengine wawili, Svetlana Tikhanovskaïa na Veronika Tsepkalo, walilazimika kukimbilia uhamishoni.

Tukio hilo la kutekwa iwapo litathibitishwa linakuja wakati mamlaka za Belarus zikionekana kuimarisha juhudi zake za kujaribu kuyavunja maandamano yanayozidi kupata nguvu.

Mkosoaji mkubwa wa rais Alexander Lukanshenko, Sviatlana Tsikhanoviskaya amelitaja tukio hilo la kutekwa kama jaribio la mamlaka la kudhoofisha uratibu wa baraza la upinzani na kuwatisha wajumbe wake.

Msemaji wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Peter Stano amesema umoja huo una taarifa kuhusu madai ya kutekwa kwa mwanaharakati huyo pamoja na wanaharakati wengine wa kisiasa. Amesema, kimsingi kile wanachokishuhudia ni mwendelezo wa ukandamizaji unaofanywa na mamlaka dhidi ya raia na kuelezea wasiwasi kuhusu kuendelea kwa hatua hizo zinazochukuliwa kwa mirengo ya kisiasa. Akasema, hilo halikubaliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.