Pata taarifa kuu
CHINA-HWO-AFYA

Coronavirus: Mkuu wa WHO aitisha kikao kipya cha dharura

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kwamba hakuna kikwazo kutoka China katika kupambana dhidi ya ugonjwa hatari unaofahamika kama Corona.

Mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus, amesema amevutiwa sana na jitihada kubwa zinazofanywa na Beijing kwa kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo hatariunaofahamika kama Corona.
Mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus, amesema amevutiwa sana na jitihada kubwa zinazofanywa na Beijing kwa kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo hatariunaofahamika kama Corona. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii mkurugenzi wa shirika hilo alizuru China kwa ziara ya siku mbili kujua kinaoendelea kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus, amesema amevutiwa sana na jitihada kubwa zinazofanywa na Beijing kwa kupambana dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo hatari, ambao umeendelea kuzua hofu ulimwenguni.

Hata hivyo vifo na kesi za maambukizi ya ugonjwa huo zinaendelea kuongezeka.

WHO imeonya kuwa kuna hatari ugonjwa huo uwe janga kubwa kimataifa.

Shirika hilo limeelezea wasiwasi wake kuhusu maambukizi baina ya binadamu nje ya China. Kamati ya dharura ya WHO inatarajia kukutana tena Alhamisi hii ili kuamua kama itaagiza kuzindua tahadhari ya afya kiulimwengu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.