Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Coronavirus: Raia wa kigeni waanza kuondolewa katika mji wa Wuhan

Nchi mbalimbali barani Asia zimeanza kuondoa raia wao nchini China kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari unaofahamika kama Corona. Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo inaendelea kuongezeka pamoja na kesi za maambukizi ya ugunjwa huo, ambao umeendelea kutia wasiwasi ulimwenguni.

Des agents en tenue de protection s'affairent autour d'un avion en provenance de Wuhan, le 29 janvier 2020.
Des agents en tenue de protection s'affairent autour d'un avion en provenance de Wuhan, le 29 janvier 2020. Kyodo via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tayari Japan na Marekani wamewaondoa mamia ya raia wao katika mji wa Wuhan, mji unaopatikana katikati mwa China.

Japan na Marekani ni nchi mbili pekee ambazo zimeanza kuondoa raia wao Jumanne na Jumatano kutoka mji wa Wuhan, kitovu cha mlipiko wa ugonjwa huo unaofahamika kama Corona, mji unaondelea kukabiliwa na hatua za kuzuia maambukizi mpya tangu Januari 23, hatua ambzo zilichukuliwa na viongozi wa China.

Nchi zingine, kama vile Australia, Korea Kusini au Uhispania zinatarajia kujiunga na nchi hizo mbili kwa kuwaondoa raia wao kwa wiki nzima, licha ya mapendekezo ya Shirika la Afya Ulimwenguni ambalo limeamua kwamba operesheni kama hiyo haikuwa lazima.

Mkuu wa WHO ambaye alizuru Beijing Jumanne, alikutana na Rais wa China Xi Jinping.

Ufaransa inatarajia kufanya zoezi hilo kwa raia wake waishio Wuhan siku ya Ijumaa wiki hii, kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Ufaransa Agnès Buzin na watawekwa karantini watakapo wasili nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.