Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Virusi vya Corona China: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 81

Serikali ya China imesema idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, vimefikia 81 na wengine zaidi ya 2,700 wameambukizwa, huku mkoa wa Hubei ukielezwa kuathirika zaidi.

Maandamano yalitokea Hong Kong katika kitongoji ambacho serikali inapanga kupanga kuhamisha wafanyakazi wa hospitali.
Maandamano yalitokea Hong Kong katika kitongoji ambacho serikali inapanga kupanga kuhamisha wafanyakazi wa hospitali. REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Maambukizi haya, yameendelea kuzua wasiwasi nchini humo na kwingineko duniani, huku mataifa ya ulimwengu yakichukua tahadhari kwa watu wanaotokea nchini China, kuepuka kusambaa kwa virusi hivyo.

Mkoa wa Hubei pekee, umerekodi watu 769 ambao wanasumbiliwa na virusi hivi, huku mmoa wa Hainan nao ukiripoti kifo cha kwanza, baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 80 kupoteza maisha.

Mataifa mengine ambayo viruso hivi vimeripotiwa ni pamoja na Korea Kusini, Thiland, Japan, Ufransa, Marekani miongoni mwa mengine.

Virusi hivi, vinapatikana kwa wanyamapori na dalili zake ni pamoja na kuwa na joto kupita kiasi, kukohoa na kupata shida ya kupumua.

Shirika la afya duniani, linasema kuepusha virusi hivi kusambaa watu wanawe mikono kwa sabuni na maji safi lakini pia, kufunika midomo yao wakiwa karibu na mtu anayepiga chafya au kukohoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.