Pata taarifa kuu
MALAYSIA-UCHAGUZI-SIASA

Upinzani washinda uchaguzi Malaysia

Malaysia imepata kiongozi mkongwe zaidi duniani aliyechaguliwa. Mahathir Mohamad , Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, amepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi mkuu uliofanyika katika taifa hilo.

Mahathir Mohamad, mwenye umri wa miaka 92, ameshinda uchaguzi nchini Malaysia, akiongoza muungano wa upinzani.
Mahathir Mohamad, mwenye umri wa miaka 92, ameshinda uchaguzi nchini Malaysia, akiongoza muungano wa upinzani. REUTERS/Lai Seng Sin
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala cha Barisan Nasional ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1957 kimejikuta kimeangushwa bila kutegemea. Hata hivyo chama hiki kimekuwa kikidaiwa kujihusisha na masuala ya rushwa na ufisadi.

Dr.Mahathir mwenye umri wa miaka 92, ameshinda kwa idadi ya uwingi wa kura.

Kufuatia ushindi wa Dr Mahathir, serikali imetangaza mapumnziko ya siku mbili ya kitaifa kwa siku ya Alhamis na Ijumaa.

Malaysia katika utawala uliopita imeshuhudia kupanda kwa gharama za maisha na ongezeko la visa vya utengano wa kikabila,

Waziri mkuu Najib Razak ameshindwa kufuatia kashfa nyingi zinazomkabili. Pia anahusishwa na kashfa ya kudaiwa kujipatia kiasi cha dola 700 kutoka taasisi moja ya maendeleo ya Malaysia na mamlaka zinaendelea kuchunguza kashfa hiyo.

Chama cha Barsia Basional kilitawala Malaysia kwa zaidi ya miaka 60. Wafuasi wa Dr Mahatir wanaendelea kusherehekea ushindi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.