Pata taarifa kuu
MALAYSIA-AJALI

Moto washambulia shule ya dini nchini Malaysia, watu 24 wapoteza maisha

Watu 24, wengi wao wakiwa wanafunzi wamepoteza maisha, baada ya shule yao ya dini mjini Kuala Lumpur, nchini Malaysia kushumbuliwa kwa moto mapema asubuhi Alhamisi hii, mamlaka amesema.

Moto wateketeza shule ya dini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, siku ya Alhamisi, na kuua watu 24, wengi wao wanafunzi.
Moto wateketeza shule ya dini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, siku ya Alhamisi, na kuua watu 24, wengi wao wanafunzi. REUTERS/Lai Seng Sin
Matangazo ya kibiashara

Moto ulianza asubuhi katika mabweni ya shule ya wavulana ya Tahfiz Darul Qur'ani Ittifaqiyah, ambapo vijana wenye umri wa miaka 13 hadi 17 walikua wakijifunza Qur'ani, amesema mkuu wa polisi wa Kuala Lumpur, Amar Singh.

Mamlaka inaamini kwamba umeme ndio chanzo cha janga hilo.

Wanafunzi walishindwa kutoka katika mabweni kutokana na moto huo ambao ulikua ukiwaka kwa kasi. Mashahidi wanasema jengo hilo lilikua na mlango mmoja tu. Taarifa hii imethibitishwa na Amar Singh, Mkuu wa polisi katika mji wa Kula Lumpur.

Miili ya wanafunzi 22 na walimu wawili pengine waathirika kwa kukosa hewa baada ya kuvuta moshi imepatikana, maafisa wa Zima Moto wametangaza Awali maafisa hao walitangaza kwamba watu 25 waliteketea kwa moto huo.

Watu wengine saba wamelazwa hospitalini na kumi na mmoja wako salama.

Hii ni moja ya ajali kubwa zaidi kutokea nchini Malaysia katika miaka ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.