Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-MALAYSIA

Pembe za Faru kutoka Msumbiji zakamatwa nchini Malaysia

Maafisa nchini Malaysia wamekamata pembe 18 za Faru zilizosafirishwa kutoka Msumbiji. 

Pembe za ndovu zilizonaswa jijini  Bangkok, Thailand, April 27, 2015.
Pembe za ndovu zilizonaswa jijini Bangkok, Thailand, April 27, 2015. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa pembe hizo zenye uzito wa kilo 51.4 zimeelezwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 3.1.

Hii inaonesha kuwa Malaysia inaendelea kuwa soko la pembe ya faru na ndovu kutoka barani Afrika katika siku za hivi karibuni.

Pembe za faru zimekuwa zikitumiwa kutengeneza dawa kwa muda mrefu lakini pia kutengeneza vikombe maalum.

Hata hivyo biashara imepigwa marufuku ili kuzuia kuuawa kwa wanyama kama Faru, na ndovu.

Mwezi Aprili mwaka uliopita, Malaysia iliharibu tani 9.5 za pembe za ndovu  ambazo zilikuwa zimekamatwa na kuhifadhiwa kwa miaka kadhaa.

Kati ya mwaka 2011 na 2014, bunge nchini Malaysia lilitangaza kuharibu pembe za ndovu na faru 4,624.

Mwezi uliopita, Shirika la Save the Elephants lilitangaza kushuka kwa bei ya pembe za ndovu dalili  za kushinda vita dhidi ya uwindaji haramu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.