Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Polisi yafaulu kuondoa wakimbizi katika kambi ya Manus nchini Australia

Polisi ya Papua imetangaza mapema leo Ijumaa kwamba wamewaondoa wakimbizi wote katika kambi ya Manus nchini Australia, na hivyo kuhitimisha wiki tatu ya mvutano na mamia ya watu wanaotafuta hifadhi ambao walikuwa wamejificha.

Polisi wa Papua New Guinea (PNG) wameingia katika kituo cha mahabusu cha wahamiaji kilichokuwa kinamilikiwa na Australia kwa azma ya kuwaondosha wanaoomba uhamiaji waliosalia.
Polisi wa Papua New Guinea (PNG) wameingia katika kituo cha mahabusu cha wahamiaji kilichokuwa kinamilikiwa na Australia kwa azma ya kuwaondosha wanaoomba uhamiaji waliosalia. AAP/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ya polisi ambayo ilianza Alhamisi, imeendelea leo Ijumaa, huku polisi wakijihami kwa vyuma na hivyo kufaulu kuwaondoa wahamiaji katika kambi hiyo na kuwasafirisha katika vituo vipya viwili.

"Kati ya saa 9:00 asubuhi na 10:00 asubuhi (sawa na saa sita usiku sa za Afrika Mashariki), wahamiaji wote walikua wameondolwaa," Dominic Kakas, afisa mkuu wa polisi kutoka Papua New Guinea, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Kwa sasa hakuan mkimbi hata mmoja katika kambi hiyo, askari wamedhibiti kambi yao," Bw. Kakas ameongeza.

Chini ya sera tata, Australia iliwashikilia watu wanaoomba uhamiaji wanaowasili kwa boti kwenye kambi katika visiwa cha Manus na Nauru, ambalo ni taifa dogo le neo la Pacific.

Australia ilifunga kituo hicho cha kisiwa cha Manus baada ya mahakama ya PNG kuamua kuwa kilikuwa ni kinyume cha sheria, na kuwataka wanaoomba uhamiaji kuhamia kwenye vituo vingine vya wanaoomba uhamiaji vilivyopo kwenye maeneo mengine ya kisiwa hicho.

Australia imekua ikikosolewa kwa miaka kadhaa kwa sera yake ngumu dhidi ya wahamiaji haramu wanaojaribu kuwasili katika pwani zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.