Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-WAKIMBIZI

Trump aweka vikwazo vipya kwa wakimbizi kutoka nchi 11

Marekani inatazamia kusimamisha kwa muda taratibu kukubaliwa kwa wakimbizi kutoka nchi kumi na moja "zinazochukuliwa hatari na utawala wa Donald Trump. Hata hivyo wakimbizi kutoa nchi nyiungibe wamekubaliwa kuendelea kuishi nchini Marekani, kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump achukua hatua nyingine dhidi ya waimbizi kutoka nchi 11.
Rais wa Marekani Donald Trump achukua hatua nyingine dhidi ya waimbizi kutoka nchi 11. /REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hati iliyotumwa siku yaJumanne na utawala wa Trump katika bunge la Congress kabla ya kuwasilishwa kwa sera mpya kuhusu mapokezi kwa wakimbizi, Washington pia imesimamisha kwa muda mpango wa kuunganisha familia ambao baadhi ya wakimbizi wamekua wakihudumiwa.

Tangazo la hatua hii mpya inakuja huku kukiwa na agizo la Donald Trump linaloagiza kusimamishwa kwa muda kwa taratibu za kukubaliwa kwa wakimbizi wengi kuendelea kuishi nchini Marekani wakati ambapo muda wa siku 120 waliopewa wakambizi hao ulimalizika siku ya Jumanne Oktoba 24. Rais wa Marekani alisaini agizo jipya linaloidhinisha kuanza kwa taratibu za kukubaliwa kwa baadhi ya wakimbizi kuendelea kuishi nchini Marekani.

"Tunaendelea kuwa wasiwasi kuhusu zoezi hili la kukubalia kuendelea kuishi nchini Marekani watu kutoka nchi kumi na moja," kuliandikwa kwenye hati hiyo, huku ikiongezwa kuwa serikali itajadili kwa muda wa siku 90 uwezekano wa hatua za udhibiti zaidi "ili kuhakikisha kwamba utaratibu wa kukubaliwa kwa wakimbizi kutoka nchi hizi si tishio kwa usalama na ustawi wa Marekani. "

Tangu kuchukua hatamu ya uongozi mnamo mwezi Januari, Rais Donald Trump alisaini agizo kadhaa zinazopiga marufuku watu kutoa nchi zenye Waislamu wengi kuingia nchini Marekani. Agizo zote hizo zimezuiliwa na mahakama kwa sababu zinaoneka kuwa ni zenye misingi ya kibaguzi.

Nchi 11 zinazochukuliwa na utawala wa Trump kama nchi "hatari", ni Korea ya Kaskazini, Misri, Iraq, Iran, Libya, Mali, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Syria na Yemen, na Wapalestina wanaoishi katika nchi hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.