Pata taarifa kuu
MAREKANi-TRUMP-WAHAMIAJI

Agizo la Trump kuhusu wahamiaji lazuiliwa tena na mahakama

Toleo la hivi karibuni la agizo dhidi ya wahamiaji la rais wa Marekani Donald Trump limezuiliwa na mahakama saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa Jumanne hii 17 Oktoba. Agizo hilo lilikua likilenga raia kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi.

Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House, Oktoba 17, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House, Oktoba 17, 2017. REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White Houte ambayo inajaribu kushinikiza kutekelezwa kwa agizo hilo tangu mwezi Januari mwaka huu, inatazamia kukata rufaa.

Rais Donald Trump amepata pigo jingine jipya baada ya agizo lake kuhusu wahamiaji kuzuliwa na mahakama. Hivi ni vita vinavyoendelea kati ya Donald Trump na vyombo vya sheria nchini Marekani. Rais wa Marekani tayari amerekebisha agizo lake mara tatu, lakini kila anaporekebisha mahakama inafutilia mbali na kuzuia utekelezaji wake.

"Toleo la tatu la agizo la Trump lina makosa kama lili lililotangulia," ameandika Jaji wa Hawaii ambaye aliagiza siku ya Jumanne kuzuiliwa kwa utekelezaji wa agizo hilo. Kabla ya kufafanua: " lina ubaguzi wenye misingi ya utaifa", matarajio yaliyotokana na "kanuni za msingi za taifa hili".

Raia kutoka Yemen, Syria, Libya, Iran, Somalia na Chad wataendelea kupata visa kwa kuingia Marekani. Jaji, kwa upande mwingine, aliruhusu hatua inayolenga raia kutoka Korea Kaskazini na viongozi wa serikali ya Venezuela.

"Hukumu hii yenye makosa ya hatari imedhoofisha jitihada za rais Trump kwa kulinda wananchi wa Marekani, " ikulu ya White House imejibu kabla ya kuthibitisha imani yake kwa mfumo wa mahakama, huku ikiongeza serikali itakata rufa haraka sana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.