Pata taarifa kuu
MAREKANi-TRUMP-WAHAMIAJI

Trump: hakuna muafaka uliofikiwa na wabunge wa Democrats kuhusu kuwalinda wahamiaji

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakuna makubaliano yoyote rasmi yaliyofikiwa na wabunge wa Democrats kuhusu hatua za kuchukua kuwalinda wahamiaji vijana walio chini ya mkataba wa DACA unaowalinda dhidi ya kufurushwa nchini humo.

Donald Trump akijibu maswali ya wanahabari kabla ya kuzuru Floride iliyokumbwa na kimbunga Irma, Septemba 14, 2017.
Donald Trump akijibu maswali ya wanahabari kabla ya kuzuru Floride iliyokumbwa na kimbunga Irma, Septemba 14, 2017. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema hakuna muafaka uliofikiwa ingawa wamekubaliana hatua za kiusalama zitakazochukuliwa kwenye mipaka na sasa wanasubiri kupigiwa kura.

Awali rais Trump alisisitiza kuwa amri yake ya kufuta sheria ya DACA inayowalinda wahamiaji vijana haina nia mbaya kwakuwa bado anwapenda vijana hao.

Wabunge wa Democrats wameapa kukwamisha hatua zozote za kuwahujumu wahamiaji walioingia nchini humo wakiwa wadogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.