Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yasema iko tayari kukabiliana na Marekani

Korea Kusini imesema haitishwi na mpango wa serikali ya Marekani kutuma manuari yake ya kivita karibu na mpaka wake.

Jaribio la kombora nchini Korea Kaskazini hivi karibuni
Jaribio la kombora nchini Korea Kaskazini hivi karibuni Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Pyonyang imesema iko tayari kwa vita. Wizara ya mambo ya nje nchini humo imeeleza kuwa  Marekani inaonekana ina mpango wa kutaka kuivamia.

Hivi karibuni, rais wa Marekani Donald Trump alisema nchi yake ina uwezo wa kukabiliana na Korea Kaskazini bila ya kupata msaada wa China.

Miaka ya hivi karibuni, Pyongyang imekuwa ikijaribu silaha zake za nyuklia ambazo zinahofiwa kuwa zinaweza kufika katika ardhi ya Marekani.

Mataifa jirani kama Korea Kusini na Japan yameendelea kulalamikia majaribio hayo yakisema  yanahatarisha usalama wao, huku China ikionekana kuunga mkono Korea Kaskazini.

Kumekuwa na ripoti kuwa Korea Kaskazini huenda ikajaribu tena silaha zake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.