Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea Kaskazini lashindwa katika jaribio jipya la kombora

Kwa mujibu wa vyanzo vya ulinzi nchini Korea Kusini, Korea Kaskazini imeshindwa katika jaribio jingine jipya la kombora. Vyanzo hivyo vinabaini kamba Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora lakini likafeli.

Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora lakini likafeli.
Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora lakini likafeli. U.S. Department of Defense, Missile Defense Agency/Handout via R
Matangazo ya kibiashara

Haijafahamika ni makombora mangapi ambayo yalitakiwa kurushwa au yalikua ya aina gani, lakini lakufahamu tu ni kwamba jaribio hilo limefeli.

Maafisa wa usalama nchini Korea Kusini wanasema Korea kaskazini ilijaribu kurusha kombora hilo angani kutoka mji wa Wonsan, pwani ya mashariki.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulipiga marufuku Korea Kaskazini kufanya majaribio yoyote ya kurusha makombora au majaribio ya nyuklia lakini nchi hiyo imeendelea kukaidi agizo hilo.

Itafahamika kwamba mwezi huu wa Machi, Korea Kaskazini ilirusha makombora manne angani ambayo yalipaa kwa umbali wa kilomita 1,000 na kuanguka maeneo ya bahari yanayomilikiwa na Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.