Pata taarifa kuu
UNSC-KOREA KASKAZINI-USALAMA

UNSC yalaani kitendo Korea Kaskazini cha kurusha makombora angani

Hata kabla ya mkutano wake wa dharura uliopangwa kufanyika Jumatano hii, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha makombora, na hivyo kuelezea wasiwasi wake kuhusu "tabia sugu ya vurugu" ya Pyongyang.

Uzinduzi majaribio ya Korea Kaskazini ya kurusha makombora ya masafa marefuwa. Picha hii imetolewa  na KCNA, Machi 7, 2017
Uzinduzi majaribio ya Korea Kaskazini ya kurusha makombora ya masafa marefuwa. Picha hii imetolewa na KCNA, Machi 7, 2017 AFP
Matangazo ya kibiashara

Shutma hizi zinatokana na Nakala iliyoandikwa na Umoja wa Mataifa, nakala ambayo imepitishwa bila kupingwa na wajumbe kumi na tano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, licha ya mvutano kati ya Washington na Beijing unaohusu kuanza kupelekwa nchini Korea Kaskazini kwa chombo cha ulinzi wa makombora cha Marekani kiitwacho THAAD.

Katika barua yake, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini kuwa ni "ukiukwaji mkubwa" wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na kuahidi "kuchukua hatua zaidi muhimu" kwa kuiadhibu Pyongyang.

Nchi kumi na tano wanachama wa Baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa zitnatazamiwa kukutana Jumatano gii asubuhi (kuanzia saa 9:00 alaasiri saa za kimataifa) mjini New York, kwa ombi la Marekani na Japan, kujadili uzinduzi wa makombora manne ya masafa marefu uliofanywa Jumatatu wiki hii ambao ni sehemu, kwa mujibu wa Pyongyang, mazoezi kwa minajili ya kushambulia kambi za jeshi la Marekani nchini Japan.

Itafahamika kwamba makombora matatu miongoni mwa makombora yaliyorushwa yalianguka katika bahari, karibu na Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.