Pata taarifa kuu
UNSC-KOREA KASKAZINI

UNSC yashindwa kuchukua uamuzi dhidi ya Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonyesha udhaifu wake Jumanne hii wa kushindwa kulaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha makombora ya masafa marefu Jumatatu wiki hii, wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ametoa wito wa kuimarisha mpango wake wa nyuklia.

Jaribio la kombora ya masafa marefu lililorushwa kutoka manowari ya jeshi la Korea ya Kaskazini.
Jaribio la kombora ya masafa marefu lililorushwa kutoka manowari ya jeshi la Korea ya Kaskazini. KCNA/File Photo via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii, Pyongyang ilirusha makomboraya masafa marefu katika pwani yake ya mashariki, operesheni ambayo mara moja ilishtumiwa na Japan, Seoul na Marekani.

Baada ya saa ya mashaurianokatika kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mabalozi wa nchi hizi tatu wameelezea mbelea ya vyombo vya habari kwamba wamelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini.

Wameelezea matumaini yao kuwa nchi 15 za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hivi karibuni litatoa taarifa ya pamoja, kama walivyofanya mwishoni mwa mwezi Agosti kwa kitendo kama hiki cha Korea Kaskazini.

"Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaendelea kuifanyia kazi taarifa hii, " balozi wa China, Liu Jieyi, amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.