Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI

Marekani yasema haitasita kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, amesema kuwa nchi yake haitasita kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwa nchi hiyo itaendelea kuwa tishio zaidi kwa usalama wa dunia kutokana na utengenezaji wa silaha za nyuklia, akionya kuwa sera ya uvumilivu wao inaelekea kuisha.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Rex Tillerson.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Rex Tillerson. REUTERS/Kevin Lamarque/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe wake ambao unaonekana ni mabadiliko ya sera ya Marekani kwenye taifa hilo lililotengwa na dunia, waziri Rex amesema ni lazima utawala wa Korea Kaskazini uachane na majaribio ya makombora na mpango wake wa nyuklia.

"Ukweli ni kuwa hatupendi kuchukua hatua hii, na kutufanya tutumie jeshi," lakini akaongeza kuwa "Ikiwa nchi ya Korea Kaskazini haitaachana na mpango wake na ukafikia kiwango cha juu, basi suala la kutumia jeshi litawekwa mezani."

"Sera yetu ya uvumilivu imeshaisha," amesema Tillerson kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Seul, Korea Kusini akiwa na mwenzake Yun Byung-Se.

"Tunatumia njia za kidiplomasia, usalama, na hali ya uchumi. Lakini kifupi yote haya yanawezekana."

Rex amesema kuwa sera ya uvumilivu ilikuwa inatumiwa na utawala wa rais Barack Obama, baada ya nchi hiyo kupiga hatua katika kuachana na mpango wake wa nyuklia.

Ziara ya Tillerson kwenye bara la Asia na has akwenye nchi ya Korea Kusini, ni ya pili kuifanya kwenye bara hilo na ni kauli ya kwanza kuitoa kuhusu mzozo wa Korea Kaskazini.

Matamshi yake ya Ijumaa ya Machi 17, ameyatoa ikiwa ni siku moja tu imepita toka aliposema akiwa mjini Tokyo Japan kuwa, miaka 20 ya juhudi ya kuifanya Korea Kaskazini isiendelee na mpango wake, zimeshindikana na juhudi mpya zinahitajika.

Nchi ya Korea Kaskazini imekuwa kwa muda mrefu ikijitahidi kuwa miongoni mwa mataifa yenye silaha za nyuklia duniani na ilifanya jaribio lake la kwanza mwaka 2006. Majaribio manne zaidi yalifuatia, majaribio mawili yakifanyika mwaka uliopita.

Tillerson ameseme kuwa nchi ya Korea Kaskazini kuachiwa iendelee kuwa na kiwango kikubwa cha teknolojia ya nyuklia sio jambo sahihi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.