Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI

Wabunge Korea Kusini wataka kura ya kumuondoa rais Park ifanyike Desemba 9

Kura ya kumuondoa madarakani rais wa Korea Kusini huenda ikafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao, taarifa ya bunge la nchi hiyo imethibitisha.

Rais wa Korea Kusini, Park Geun-Hye.
Rais wa Korea Kusini, Park Geun-Hye. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Idadi kadhaa ya wabunge wa chama tawala wameunga mkono kampeni ya vyama vya upinzani kumuondoa madarakano rais Park Geun-Hye, anayekabiliwa na kashfa ya matumizi mabaya ya ofisi inayomuhusisha na rafiki yake Choi Soon-Sil, ambaye anadaiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwa rais.

"Tutaomba kura ya kumuondoa rais madarakani ifanyike Desemba 2 na sio zaidi ya Desemba 9," alisema Woo Sang-Ho kiongozi kutoka kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Hata hivyo wabunge wa chama tawala nchini Korea Kusini wanataka kura hiyo ifanyike Desemba tisa kuamua hatma ya rais Hye.

Người dân Hàn Quốc biểu tình đòi tổng thống Park Geun Hye từ chức, Seoul, ngày 19/11/2016.
Người dân Hàn Quốc biểu tình đòi tổng thống Park Geun Hye từ chức, Seoul, ngày 19/11/2016. REUTERS/Kim Hong-Ji

Upinzani umekuwa ukisita kuupitisha muswada huo kwa kupata robo tatu ya kura licha ya kuwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani kutoka vyama vingine, katika bunge lenye wawakilishi 300.

Hata hivyo harakati za upinzani zilipata nguvu kubwa baada ya aliyekuwa kinara wa wabunge wa chama tawala bungeni, Kim Moo-Sung, kudai kuwa anawaunga mkono viongozi wa upinzani na kutaka rais Park aondoke madarakani akidai amekiuka katiba ya nchi.

Ikiwa kura hii itafanikiwa kupita, itakuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12, kuona bunge la Korea Kusini linapiga kura kumuondoa rais madarakani.

Rais Park tayari ameomba radhi kwa uma na kuahidi kuwa atakuwa tayari kuhojiwa na tume iliyoundwa kumchunguza pamoja na kuundwa kwa tume huru itakayoundwa na bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.