Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-SIASA-JAMII

Rais wa zamani wa Korea Kusini Kim Young-sam afariki

Rais wa zamani wa Korea Kusini Kim Young-sam, ambaye katika mwaka wa 1993 alikua rais wa kwanza raia baada ya miaka 30 ya utawala wa kijeshi, amefariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 87, vyanzo hospitali vimebaini.

Rais wa zamani wa Korea Kusini Kim Young-sam jijini Seoul Januari 6, 1995.
Rais wa zamani wa Korea Kusini Kim Young-sam jijini Seoul Januari 6, 1995. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Kim Young-sam, ambaye aliongoza Korea Kusini kati ya mwaka 1993 na 1998, alikua anaumwa maambukizi ya damu. Alilazwa hospitali siku chache kabla ya kifo chake kutokana na homa kali, mkurugenzi wa hosopitali kuu ya taifa ya Seoul, Oh Byung-Hee, amewaambia waandishi wa habari.

Matukio mawili makubwa yalishuhudiwa katika utawala wake: kmgogoro wa kwanza wa nyuklia na Korea Kaskazini mwaka 1994 na kusainiwa kwa mpango wa uokoaji wa dola bilioni 58 pamoja na Shirika la Fedha Duniani (IMF), wakati wa mdororo wa kifedha barani Asia wa mwaka 1997-1998.

Mwanaharakati muhimu wa utetezi wa Demokraisia, alipewa mara mbili kifungo cha nyumbani kwa jumla ya muda wa miaka miwili mapema katika miaka ya 1980.

Alikuwa mgombea katika uchaguzi wa kwanza huru wa urais nchini humo mwaka 1987, lakini dhidi ya upinzani uliogawanyika, afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika jeshi Roh Tae-Woo ndiye alichaguliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.