Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USALAMA

Seoul yataka msamaha kutoka Pyongyang, mazungumzo yanaendelea

Korea ya Kusini imeonya Jumatatu kwamba haitasitisha vita vya propaganda kwenye mpaka wake kama Pyongyang haitaomba radhi, wakati ambapo nchi hizo mbili hasimu zikiendelea na mazungumzo ya kasi ili kumaliza mvutano huo wa kijeshi kati ya mataifa hayo mawili.

Wanajeshi wa Korea Kusini, Agosti 24, 2015 kwenye mpaka na Korea ya Kaskazini
Wanajeshi wa Korea Kusini, Agosti 24, 2015 kwenye mpaka na Korea ya Kaskazini AFP/YONHAP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ametoa onyo hilo wakati wawakilishi wakuu kutoka pande zote mbili wamekua wakikutana katika kijiji kiliyo kwenye mpaka cha Panmunjom kujadili jinsi ya kupatia ufumbuzi mgogoro huo. Katika kijiji cha Panmunjom ndipo kulisainiwa mkataba wa kusitisha vita vya miaka ya 1950 hadi 1953.

Hata hivyo, matumaini ya kupatikana kwa ufumbuzi yalikuwepo, licha ya kuwa Pyongyang ainaituhumu Seoul kudhoofisha mazungumzo kwa kufanya harakati za kijeshi.

Korea ya Kaskazini inatakiwa " kuomba msamaha wa wazi " kwa yale yote Seoul inaona kama ni mfululizo wa " uchokozi" na "kuhakikisha " kwamba pyongyang haitajirudia kwa chokochoko hizo, amesema Rais wa Korea Kusini wakati wa mkutano na washauri wake.

Pyongyang imeanzisha mgogoro wa sasa kwa " shughuli uchokozi ", ameongeza rais wa Korea Kusini.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini, Pyongyang imeongeza mara mbili idadi ya wanajeshi wake kwenye mpaka na Korea Kusini, na imepeleka theluthi ya nyambizi zake, sawa na vyombo vya kijeshi zaidi ya hamsini nje ya kambi zake za jeshi.

Wizara ya Ulinzi pia imesema kuwa imekua ikifuatilia kwa karibu safari za nenda-rudi za meli za Korea Kaskazini. Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap , Korea ya Kaskazini imepeleka vyombo kadhaa vya majini (amphibious) viliobeba vikosi maalum hadi katika kambi ya jeshi la majini iliyoko kilomita sitini na " Mstari unaogawa Korea hizo mbili " (NLL), ambao unatambuliwa na Korea Kusini kama mpaka wa nchi hizi mbili.

Korea ya Kaskazini inakubali mpaka mwingine wa bahari, ambao ni msati unaogawa eneo la majeshi kutoka nchi hizo mbili.

" Korea Kaskazini ina tabia ya kinafiki wakati majadiliano yakiendelea. Tunaichukulia hali hii kwa umakini mkubwa ", amesema mmoja wa wasemaji wa seriali ya Korea Kusini.

Mazungumzo ya Panmunjom yanaongozwa na mshauri wa usalama wa taifa kutoka Korea Kusini, Kim Kwan-Jin, na mwenzake kutoka Korea Kaskazini, Hwang Pyong-So, ambaye ni mshirika wa karibu wa Kim Jong-Un.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.