Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UCHAGUZI

David Nakhid, awania urais wa FIFA

David Nakhid, nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Trinité-et-Tobago, ameliambia Jumatano wiki hii mjini Beirut shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa atawania katika uchaguzi wa urais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA.

David Nakhid, nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Trinite-et-Tobago, katika mkutano na waandishi wa habari, Septemba 28, 2015 jijini Beirut.
David Nakhid, nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Trinite-et-Tobago, katika mkutano na waandishi wa habari, Septemba 28, 2015 jijini Beirut. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Nakhid, mwenye umri wa miaka 51, ni mgombea rasmi wa tatu katika kumrithi Sepp Joseph Blatterkwenye uongozi wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), baada ya Michel Platini (kwa sasa amesimamishwa kwa muda wa siku 90 katika shughuli yoyote inayohusiana na mpira wa miguu) na Prince Ali wa Jordan.

" Niliwasilisha barua yangu ya kugombea wiki iliyopita mjini Zurich, ninaungwa mkono na taasisi tano wanachama wa FIFA, lakini ni bora kutotajwa majina kwa sasa ", Nakhid amelieleza shirika la habari la Ufaransa la AFP katika mji mkuu wa Lebanon, ambako anaongoza shule ya soka.

" Nafasi ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) iliyo wazi inapaswa kuchukuliwa na mtu mwenye uchuzi na uwelewa wa mambo ya mchezo, hususan soka, ili kuweka sawa na kufuatilia kwa karibu mchezo unaopendwa duniani kupitia mabadiliko ambayo kila mtu anataka, lakini hakuna aliyewahi kuyatekeleza, kwani mabadiliko haya muhimu yanapaswa kukabili mfumo na sheria zake, hapana watu, " Nakhid ameomba.

David Nakhid, ambaye alicheza katika nafasi ya kiungo wa kati, alianza kazi yake ya soka mwaka 1990 katika micchuano ya Ubelgiji katika mji wa Waregem, kabla ya kwenda Uswisi (katika mji wa Grasshopperi Zurich) mwaka 1992. Baada ya msimu mmoja nchini Ugiriki, mwaka 1994-1995, alimaliza kazi yake mwaka 2005 nchini Lebanon.

Kimataifa, alivaa mara 35 jezi za Trinite-et-Tobago kati ya mwaka 1992 na 2004, kwa mabao manane aliofunga.

Uchaguzi wa urais wa FIFA umepangwa kufanyika Februari 26, na tarehe ya mwisho ya maombi ni Jumatatu wiki ijayo.

Wagombea wengine wanaotazamiwa kabla ya tarehe hiyo ya mwisho ni rais wa Soka barani Asia, ni Sheikh Salman bin Ibrahim Al Khalifa, Makamu wa Rais wa FIFA, mwenye umri wa miaka 49, ambaye ni kutoka Bahraini pamoja na raia wa Afrika Kusini, Tokyo Sexwale, mfanyabiashara na rafiki wa zamani aliyefungwa katika chumba kimoja cha jela na Nelson Mandela. Sexwale ana umri wa miaka 62. Aliteuliwa mwaka huu kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi ya FIFA kwa Israel na Palestina.

Mgombea mwingine anaweza kutokea, ni Mfaransa, Jérôme Champagne, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa FIFA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.