Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-MKUTANO

FIFA yapania kufanya mageuzi

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeamua kuwa tarehe ya uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo itasalia ile ile, Februari 26, 2016. FIFA pia imebaini kuwa kugombea kwa Michel Platini, raia wa Ufaransa, hakutajadiliwa kwa kipindi chote cha kusimamishwa kwake cha siku 90.

Picha iliyotolewa na Kamati tendaji ya Fifa katika mkutano wa dharura uliofanyika Zurich, Oktoba 20, 2015.
Picha iliyotolewa na Kamati tendaji ya Fifa katika mkutano wa dharura uliofanyika Zurich, Oktoba 20, 2015. AFP/FIFA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya tendaji hata hivyo imejadili mageuzi makubwa, ikiwa ni pamoja na kueweka kikomo kuhusu umri na muhula kwa raia wa Shirikisho la Soka Duniani atakaye chaguliwa.

Bado haijulikani kama Michel Platini, raia wa Ufaransa aliyesimamishwa hadi Januari 5, 2016 na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya FIFA, atagombea kwenye nafasi ya urais waShirikisho la Soka Duniani.

Lakini jambo la uhakika ni kuwa uamzi huu wa kutobadili tarehe ya uchaguzi (Februari 26, 2016) , uliyotangazwa Oktoba 20, 2015 na kamati tendaji, ambayo ndio "serikali" ya FIFA, haisaidii masuala ya rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA).

Hakika, suala la kugombea kwa Michel Platini, mchezaji wa zamani wa soka, halitajadiliwa kwa kipindi chote cha kusimamishwa kwake cha siku 90, Tume ya Uchaguzi ya FIFA imebaini. Hata hivyo, faili za wagombea zinatakiwa kuwa zimekubaliwa kabla ya Januari 26. Na wale ambao walimhukumu Platini ndio watakaojadili uhalali wake kwa kuweza kushiriki katika uchaguzi huo.

Michel Platini bado anasubiri

Michel Platini anatuhumiwa kupokea kinyume cha sheria faranga za Uswisi milioni mbili mwaka 2011 kutoka kwa Joseph Blatter, rais wa FIFA aliyejiuzulu, ambaye pia alisimamishwa kwa muda wa siku 90.

Itakumbukwa tu kwamba Michel Platini alikata rufaa kwenye Kamati ya Nidhamu na Maadili dhidi ya uamzi huo. Kama atashindwa, anawezakuwasilisha mashtaka yake kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo, taasisi kuu ya sheria ya michezo, ili uamzi wa kusimamishwa kwake "ufutwe".

Katika mkutano huo waliafikiana kuwa rais wa FIFA atakaye chaguliwa hatakuwa na zaidi ya umri wa miaka 74 na hatozidisha mihula mitatu, sawa na miaka kumi na mbili. Uamzi huu ulikuwa hata hivyo, ulikataliwa na FIFA katika miaka ya hivi karibuni. Joseph Blatter alikuwa alichaguliwa tena Mei 29, akiwa na umri wa 79 kwa muhula wa tano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.