Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-MKUTANO

Mkutano wa dharura wa kamati tendaji ya FIFA bila kuwepo Blatter au Platini

Sepp Joseph Blatter na Michel Platini hawatashiriki katika mkutano wa dharura wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA jijini Zurich Jumanne hii, lakini watawakilishwa. Huu ni mkutano wa kwanza tangu kusimamishwa kwa viongozi hawa kwenye nyadhifa zao.

Michel Platini (kulia) na Sepp Blatter, Zürich, Mei 29, 2015.
Michel Platini (kulia) na Sepp Blatter, Zürich, Mei 29, 2015. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa dharura uliamuliwa tarehe 9 Oktoba siku moja baada ya dhoruba iliyolikumba Shirikisho la Soka Duniani FIFA na kusimamishwa kwa muda wa siku 90 Blatter na Platini, ambaye alikua nafasi kubwa ya kushinda kwenye uchaguzi wa rais wa FIFA, baada ya nafasi hiyo kushikiliwa tangu mwaka 1998 na Mswisi Sepp Joseph Blatter.

Sepp Blatter na Michel Platini wanatuhumiwa kashfa ya ufisadi katika shirikisho hilo. Kabla ya uamzi wa FIFA, wawili hao walikua wakitupiana vijembe, kila mmoja akimtuhumu mwengine na kupinga kuendelea kushikilia wadhifa wowote katika taasisi za Soka ulimwenguni.

Hatua hii inakuja baada ya viongozi wa Mashtaka nchini Uswizi kumchunguza Blatter kwa tuhma za kutoa malipo yasiyokuwa rasmi kwa rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA), Michel Platini, lakini alisaini mkataba ambao haukuwa na manufaa kwa FIFA.

Awali Blatter alikanusha tuhma hizo na kusema hana hatia yoyote na hawezi kujizulu kabla ya tarehe 26 mwezi Februari mwaka ujao siku ambayo uchaguzi mpya wa FIFA utakapofanyika.

Michel Platini naye, awali alisema fedha alizolipwa alikuwa amezifanyia kazi na hajahusika na ufisadi.

Kamati imeanza kugeuza taswira: ni " Kamati tendaji ya kwanza bila mimi kuwepo tangu miaka 40 ", alisema Sepp Blatter Ijumaa wiki iliyopita kwenye Redio RROTV. Blatter alijiunga na FIFA mwaka 1975. Kukosekana kwa Blatter na Platini, vigogo wawili wa soka duniani, ni tukio la kushangaza linaloashiria mgogoro unayoikabilii taasisi ya kimataifa ya soka.

Katika mkutano huo, huenda kukajadiliwa suala la mihula, na kurejesha uaminifu katika Shirikisho la Soka Duniani FIFA, na mishahara ya viongozi wa taasisi hiyo ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.