Pata taarifa kuu
THAILAND-SHAMBULIO-USALAMA

Polisi ya Thailand yawasaka watu 3 wanaoshukiwa kuendesha shambulizi Beijing

Serikali nchini Thailand imesema inamtafuta raia wa kigeni pamoja na watu wengine wawili wanaoaminiwa kutekeleza shambulio la bomu katika eneo takatifu jijini Bangkok wiki hii na kusabisha vifo vya watu 20 wengi wao wakiwa watalii.

Mjini Bangkok shada za maua zimekua zikiwekwa kwenye eneo la shambulio.
Mjini Bangkok shada za maua zimekua zikiwekwa kwenye eneo la shambulio. REUTERS/Kerek Wongsa
Matangazo ya kibiashara

Idara ya polisi imesema kuwa mshukiwa huyo anaaminiwa kuzungumza lugha ya kigeni mbali na kiingereza.

Inashukuwa kuwa huenda mshukiwa huyo anatokea katika eneo la Mashariki ya kati au Kusini mwa bara Asia.

Serikali imetenga kitita cha Euro 25,000 kwa mtu yeyote ambaye ataweza kutoa taarifa za kupelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, ambaye polisi imemtaja kuwa mhusika mkuu wa shambulio hilo.

Inaelezwa kuwa mshukiwa huyo hakutekeleza shambulio hilo la Jumatatu pekee yake kwa mujibu wa picha za CCTV zilionekana.

Pamoja na hilo, Waziri Mkuu Prayut Chan-o-cha amesema ni mapema kufahamisha ikiwa shambulio hilo lilikuwa la kigaidi.

Hadi sasa haijafahmika ikiwa kuna kundi lolote la kigaidi lililotekeleza shambuliohilo ambalo liliwalenga watalii ambao hufika katika eneo hilo la kuabudu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.