Pata taarifa kuu
THAILAND-SHAMBULIO-USALAMA

Bomu lalipuka katikati mwa Bangkok, na kusababisha vifo vya watu wengi

Bomu limelipuka leo Jumatatu jioni katika mji wa Bangkok, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 18 na wengine wengi kujeruhiwa. Mlipuko huo umetokea kati ya mojawepo ya sehemu takatifu na maarufu zaidi na eneo la kibiashara katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok. Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi, washambuliaji walikua wamelenga raia wa kigeni.

Waokoaji wakiondoa mwili wa mwathirika wa shambulio lililotokea Bangkok, Agosti 17 mwaka 2015.
Waokoaji wakiondoa mwili wa mwathirika wa shambulio lililotokea Bangkok, Agosti 17 mwaka 2015. REUTERS/Kerek Wongsa
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea Jumatatu wiki hii saa moja usiku (saa za Thailand) karibu na Erawan Hindu,sehemu takatifu na maarufu zaidi katika mji mkuu wa Thailand, hasa kwa jamii ya wa Hindu. sehemu hiyo inapatikana katikati mwa mji mkuu wa Thailand Bangkok.

Eneo hilo la Erawan Hindu, lililoko mkabala na hoteli moja ya kifahari, pia hutembelewa na maelfu ya wabudha kila siku na ni maarufu sana kwa watalii.

Msemaji wa polisi, Prawut Thavornsiri, amebaini kwamba kilicholipuka ni bomu. “ Lakini siwezi ikasema kwa wakati huu ni bomu la aina gani, bado tunachunguza”, amesema Prawut Thavornsiri.

Ripoti ya mwisho inaeleza kuwa zaidi ya watu 18 wameuawa katika shambulio hilo, ikiwa ni pamoja na raia mmoja wa China na mwengine kutoka Ufilipino, na zaidi ya watu wengine 80 wamejeruhiwa.

Hakuna kundi hata moja ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo, lakini viongozi wamebaini kifaa hicho kililipuka kilikua kimefungwa kwenye pikipiki.

"Ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba kuna mlipuko uliotokea katikati mwa mji wa Bangkok, ambapo bomu lilitegwa kwenye pikipiki ", amehakikisha naibu mkuu wa polisi, Aek Angsananond.

Eneo hilo limezingirwa na polisi. Mwandishiwa RFI katika eneo la tukio, Arnaud Dubus ameeleza kuwa " miili mingi ya watu waliofariki iliohifadhiwa katika shuka inaonekana pembezoni mwa hekalu ".

Thailand inakabiliwa na waasi wa Kiislam katika kiwango cha wastani, waasi ambao wamekua wakiendesha harakati zao kusini mwa taifa hilo. Thailand inakabiliwa pia na uhasama kati ya pande za kisisasa kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.