Pata taarifa kuu
Thailand-SHINAWATRA-SHERIA-SIASA

Thailand: Yingluck Shinawatrwa asikilizwa mahakamani

Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Yingluck Shinawatrwa amewasili jijini Bangkok tayari kwa kuanza kusikiliza kesi inayomkabili.

waziri mkuu wa zamani wa Thailand Yingluck Shinawatra.
waziri mkuu wa zamani wa Thailand Yingluck Shinawatra. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Shinawatra ameshatakiwa na kosa la kutokuwa makini kazini wakati alipokuwa Waziri Mkuu na kusababisha kupotea kwa fedha za umma kuhusu mradi wa uuzaji wa mchele. Hata hivyo Yingluck Shinawatrwa amekanusha tuhuma dhidi yake.

Ikiwa atapatikana na kosa atafungwa jela miaka 10.

Mwaka 2014 Bi Shinawatara aliondolewa madarakani na Mahakama kwa utumizi mbaya wa madaraka.

Shinawatra amesema kesi inayomakabili imechochewa kisiasa.

Mwezi Februari mwaka 2014, waziri huyo mkuu wa zamani wa Thailand, Yingluck Shinawatra alijitokeza kwa mara ya kwanza na kujitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi na kushindwa kuwajibika kama kiongozi. Utetezi wa Yingluck ulikuja wakati ambapo tume ya kupambana na rushwa nchini humoilikua iliwasilisha kesi mahakamani, kumshtaki waziri mkuu huyo wa zamani kwa kushindwa kuwajibika na kuisababishia nchi hasara ya mamilioni ya fedha kutokana na pembejeo za kilimo cha mpunga.

Kiongozi huyo huyo wa zamani wa Thailand alikana mara kadhaa tuhuma hizo akisisitiza ni njama za kutaka kumn'goa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.