Pata taarifa kuu
NEPAL-TETEMEKO-USALAMA

Watu waodolewa chini ya vifusi wakiwa hai

Shirika la Msalaba mwekundu linasema limefanikiwa kumwokoa mvulana na mwanamke chini ya maporokomoko ya ardhi wakiwa hai karibu juma moja baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Nepal.

Shughuli za uokozi zinaendelea Kathmandu, Nepal. Kijana huyu mwenye umri wa miaka 15 ameokolewa akiwa hai kutoka chini ya vifusi jumamoja baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Nepal, Aprili 30 mwaka 2015.
Shughuli za uokozi zinaendelea Kathmandu, Nepal. Kijana huyu mwenye umri wa miaka 15 ameokolewa akiwa hai kutoka chini ya vifusi jumamoja baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Nepal, Aprili 30 mwaka 2015. REUTERS/Adnan Abidi
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa kijana huyo aliyepatikana hai ana miaka 15 pamoja na mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 20, wamesema ni muujiza kupatikana akiwa hai baada ya siku tano .

Wakati huo huo, Shirika la Msalaba mwekundi linasema vijiji na miji imeathiriwa zaidi na hakuna chochote kinachosalia.

Zaidi ya watu elfu sita wamepoteza maisha na maelfu bado hawajapatikana.

Serikali inahofia kuwa huenda idadi ya watu waliopoteza maisha ikafikia Elfu 10.

Licha ya msaada kutoka kwa wataalam wa uokozi kutoka kwa serikali ya Nepal na Jumuiya ya Kimataifa, juhud za kuwatafuta watu ambao huenda wako hai au miili hasa jijini Kathmandu zinatatizwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.