Pata taarifa kuu
NEPAL-TETEMEKO-USALAMA

Nepal: idadi ya watu waliofariki yaendelea kuongezeka

Nchini Nepal, watu wengi wamelazimika kwa mara nyingine tena kulala nje usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne Aprili 28 baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Richter 7.8 kuharibu au kuteketekeza nyumba nyingi Jumamosi usiku Aprili 25.

Mkazi wa Bhaktapur, Nepal, Jumapili Aprili 26 mwaka 2015 katika vifusi vya mji, uliyoharibiwa sehemu kubwa na tetemeko la ardhi siku moja baadae.
Mkazi wa Bhaktapur, Nepal, Jumapili Aprili 26 mwaka 2015 katika vifusi vya mji, uliyoharibiwa sehemu kubwa na tetemeko la ardhi siku moja baadae. REUTERS/Navesh Chitrakar
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko hilo la ardhi imeendelea kuongezeka, na kufikia sasa zaidi ya watu 5,000, kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Nepal ambaye ametangaza leo Jumanne siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Waziri Mkuu Sushil Koirala, amesema Jumanne Aprili 28 kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi inaweza kufikia watu 10 000.

" Hatujapokea taarifa kutoka vijiji vya mbali", amesema Sushil Koirala. Hali hii haizui Idara za serikali kupokea simu kutoka pande zote.

" Tunashindwa kuandaa shughuli za uokozi kwa pamoja katika maeneo mengi kutokana na ukosefu wa vifaa na wataalamu", amelaumu Waziri Mkuu wa Nepal. Mkurugenzi kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ameelezea ombi la Nepal kwa nchi za kigeni kwa kutuma vifaa vya dharura na timu ya matabibu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu milioni nane wameathirika na tukio hilo.

Msaada kutoka jumuiya ya kimataifa umeanza kuwasili nchini Nepal. Marekani imeongeza msaada wake kutoka dola milioni 1 hadi milioni 10. Wakati huo huo, uwanja wa ndege wa Kathmandu umezidiwa na wingi wa watu wanaotaka kusafiri ikilinganishwa na ndege zinazoleta misaada ambazo zimekua zikijaribu kutua. Jumatatu Aprili 27, ndege mbili kutoka India zimelazimika kurudi nyuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.