Pata taarifa kuu

Baada ya kifo cha Navalny, Marekani yazindua safu mpya ya vikwazo dhidi ya Urusi

Washington imetangaza siku ya Ijumaa, Februari 23, mlolongo mkubwa zaidi wa vikwazo tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Vikwazo ambavyo vinalenga zaidi ya watu 500 na mashirika kutoka nchi tofauti, pia katika kukabiliana na kifo cha mpinzani Alexeï Navalny wiki moja iliyopita.

Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na mjane na binti ya Alexeï Navalny, huko San Francisco, Februari 22, 2024.
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na mjane na binti ya Alexeï Navalny, huko San Francisco, Februari 22, 2024. © Manuel Balce Ceneta / AP
Matangazo ya kibiashara

"Vladimir Putin lazima alipe gharama kubwa kwa uchokozi wake dhidi ya Ukraine. » Hivi ndivyo Joe Biden ameandika siku ya Ijumaa asubuhi, wiki moja baada ya kifo cha Alexeï Navalny na katika mkesha wa mwaka wa pili wa kuanza kwa vita nchini Ukraine. Taarifa kwa vyombo vya habari ya Ikulu ya White House ilichapishwa mapema sana asubuhi ya leo, ikitangaza seti kubwa zaidi ya vikwazo vilivyochukuliwa hadi sasa na nchi dhidi ya Urusi, anasema mwandishi wetu wa New York, Loubna Anaki.

Kwa jumla, vikwazo vipya 500 vinalenga makampuni kutoka nchi 26, watu kutoka nchi 11, ikiwa ni pamoja na China au Ujerumani, na vinahusu sekta ya fedha ya Urusi, sekta ya ulinzi, watu mbalimbali wanaounga mkono Moscow, lakini pia watu wanaohusishwa na kifungo cha mpinzani Alexeï Navalny, ambaye alifariki wiki moja iliyopita.

Tangazo la safu hii ya vikwazo vipya pia linakuja siku moja baada ya mkutano wa Joe Biden na mke na binti wa Alexeï Navalny. Kwa undani, maafisa watatu wa Urusi ni miongoni mwa wale waliolengwa na Marekani kwa kuhusika kwao katika kifo hiki, Wizara ya Mambo y Nje ya Marekani pia imebainisha. Hii inafikisha zaidi ya 4,000 idadi ya vyombo vinavyolengwa na vikwazo vya Marekani tangu kuanza kwa vita.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.