Pata taarifa kuu

Marekani: Democrats wazindua kampeni kujaribu kurejesha kura za walio wachache

Joe Biden ameanza rasmi kampeni za uchaguzi wa mwezi Novemba. Amehutubia Wamarekani wenye asili ya Afrika. Fursa ya kukemea ukuu wa wazungu na kujaribu kurejesha upendeleo wa wapiga kura wachache. Kambi ya Democratic inazidi kuwa na wasiwasi kuhusu kutengwa kwao. Siku ya Jumanne, aRai Joe Biden alizindua kampeni inayolenga watu weusi, Walatino na Waasia hasa, miezi kumi kabla ya kura.

Rais wa Marekani Joe Biden anataka kupata kura za walio wachache kabla ya uchaguzi wa Novemba 2024.
Rais wa Marekani Joe Biden anataka kupata kura za walio wachache kabla ya uchaguzi wa Novemba 2024. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Tafiti zote zinaonyesha hili. Hata kabla ya wapiga kura wengi Waislamu kujitenga na Joe Biden kwa sababu ya uungaji mkono wake kwa Israel katika vita vya Gaza, wapiga kura wengi weusi, Latino na Asia walikuwa walijitenga na chama cha Democratic katika miezi ya hivi karibuni. Hali ya uchumi, kushindwa kupunguza madeni ya wanafunzi, hata usimamizi mbovu wa uchomaji moto misitu; kila jamii imejiwekea chuki dhidi ya kambi ya Democratic. Lakini chama kimekiri makosa yote, na kinataka kuwajibika.

Chini ya neno "POWER", kampeni hii kubwa inataka kurejesha kura hizi muhimu, hasa katika maeneo ambayo chama cha Republican kilipoteza miaka miwili iliyopita, kama vile New York. Uchunguzi unafanyika katika maeneo mbalimbali, kampeni katika lugha kadhaa (Kiingereza, Kihispania, au hata Kikorea kwa mfano), changamoto ni kuwashawishi wapiga kura hawa kunufaika na mageuzi yaliyofanywa kwa ajili ya uwezo wao wa kununua au juhudi za kulinda haki zao za kimsingi, kutokana na vitisho kutoka kwa kambi ya Republican.

Dola milioni thelathini na tano zitatolewa kwa kampeni iliyoanzishwa miezi 10 kabla ya uchaguzi. Jibu la ukosoaji unaotolewa mara kwa mara na chama kwa kuonyesha tu nia ya kuungwa mkono na walio wachache katika wiki za mwisho za kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.