Pata taarifa kuu
MAPIGANO-USALAMA

Wahindi 1,400 wakimbia mapigano kati ya makundi yenye silaha nchini Colombia

Haya yanajiri katika akaunti ya Nariño, kusini magharibi mwa nchi. Walikimbia eneo lao linaloitwa hifadhi ya Awa Sande ili kukwepa mapigano kati ya wapiganaji wa ELN na moja ya makundi yenye silaha vya Central Staff (EMC), kundi kuu lililogawanyika la waasi wa zamani wa FARC. Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea tangu Septemba 13.

Mmoja wa wapiganaji wa kundi la waasi la ELN.
Mmoja wa wapiganaji wa kundi la waasi la ELN. REUTERS - Federico Rios
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Bogota, Marie-Eve Detoeuf

Nariño ni akaunti ya milima kwenye mpaka na Ecuador. Eneo ambalo limedhibitiwa kwa muda mrefu na wapiganaji wakuu wa Farc, waliopokonywa silaha mwaka wa 2016. Na eneo ambalo linasalia kuwa la kimkakati kudhibiti usafirishaji wa kokeini. ELN na EMC ni makundi mabyo yamekuwa yakipigania udhibiti wa eneo hilo kwa miezi kadhaa. Wakulima na Wahindi ndio wanaobeba mzigo mkubwa wa vita.

Wiki hii, Wahindi kutoka eneo linaloitwa hifadhi ya Awa Sande walifika kwa mamia katika vijiji vya Samaniego na Santacruz. Miongoni mwao, wazee, wanawake wajawazito, watoto wengi. Walikimbia kwa miguu. Eneo hilo limejaa mabomu yaliyotewa ardhini . Mamlaka imewaweka wakimbizi hao katika vituo vya kawaida vya michezo. Watu hao waliolazimika kuyahama makaazi yao wanaiomba serikali msaada, magodoro, chakula. Na wanaomba kuwepo kwa Kamishna Mkuu wa Amani, Danilo Rueda, ili awe mpatanishi kati ya makundi yenye silaha. ELN na EMC yote zinashiriki katika mazungumzo magumu ya amani na serikali ya Gustavo Petro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.