Pata taarifa kuu

Colombia na Venezuela zatia saini makubaliano ya kuwatafuta waliotoweka kwenye mpaka wao

Rais wa mrengo wa kushoto wa Colombia Gustavo Petro anaendelea na maelewano yake ya kisiasa na nchi jirani ya Venezuela. Baada ya kufunguliwa kwa mipaka kati ya nchi hizo mbili, sasa ni ushirikiano usio na kifani ambao umetiwa saini ili kuhakikisha kuwa watu waliotoweka kwenye mipaka ya pamoja wanapatikana.

Daraja la Simon Bolivar kati ya Cucuta, Colombia, na San Antonio de Tachira, Venezuela.
Daraja la Simon Bolivar kati ya Cucuta, Colombia, na San Antonio de Tachira, Venezuela. AFP - EDINSON ESTUPINAN
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Medellin, Najet Benrabaa

Colombia na Venezuela zinashiriki zaidi ya kilomita 2,200 za mpaka wa pamoja. Mpaka ambapo makundi yenye silaha ya walanguzi wa dawa za kulevya, wapiganaji wa msituni na wanamgambo wameendesha shughuli zao wakati wa miongo kadhaa ya vita nchini Colombia. Matokeo: maelfu ya waathiriwa na watu waliotoweka.

Mkataba uliotiwa saini huko Bogota kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili mnamo Ijumaa Juni 30 unatoa uanzishwaji wa "njia zinazofaa zaidi na za haraka za kutafuta, kurejesha na kutambua mabaki ya binadamu kwenye eneo la Venezuela".

Kurekebisha kasoro zilizojitokeza

Pia ni mwendelezo wa sera ya ukaribu iliyoanzishwa na rais wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro mara tu alipoingia madarakani mwezi Agosti 2022. Mahusiano ya kidiplomasia yalianza tena baada ya kudorora kwa miaka kadhaa, tangu mwaka 2019 na serikali ya mtangulizi wake Ivan Duque, ambayo ilishutumu kuchaguliwa tena kwa udanganyifu kwa Nicolas Maduro.

Mbali na msako wa watu waliotoweka mpakani, nchi hizo mbili pia zimejitolea kukidhi mahitaji ya raia wao. Hii ina maana kwamba balozi za Colombia na Venezuela zitafunguliwa tena pande zote za mpaka. Kwa upande wa Colombia, balozi ndogo zitafunguliwa tena huko Caracas, Maracaibo, San Antonio del Táchira na San Cristóbal. Kwa upande wa Venezuela, balozi zitafunguliwa tena huko Bogota, Medellín, Cartagena, Barranquilla na Riohacha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.