Pata taarifa kuu

Mataifa ya Amazon yazindua mpango wa kukabiliana na ukataji miti

Mataifa manane ya Kusini mwa Amerika yanayounda msitu wa Amazon, yamezindua mpango wa pamoja, kupambana na ukataji miti ili kuhifadhi misitu, wakati wa kikao cha siku mbili nchini Brazil. 

Mpango huo umeandikwa kwenye mkataba wa maneno Elfu 10, wenye malengo ya kuendeleza maendeleo katika nchi hizo
Mpango huo umeandikwa kwenye mkataba wa maneno Elfu 10, wenye malengo ya kuendeleza maendeleo katika nchi hizo © Eraldo Peres / AP
Matangazo ya kibiashara

Wakuu hao wa nchi za Brazil, Bolivia, Colombia, Ecuador na nyingine, wamesema, mpango huo utasaidia kulinda na kuhifadhi misiti hiyo ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, wakati huu watalaam wakionya kuwa kiwango cha joto duniani, kinaendelea kupanda na hali itakuwa mbaya katika siki zijazo, iwapo hatua hazitochukuliwa. 

Mpango huo umeandikwa kwenye mkataba wa maneno Elfu 10, wenye malengo ya kuendeleza maendeleo katika nchi hizo lakini pia, kupambana na makundi ya uhalifu yanayohusika na biashara haramu ya ukataji miti. 

Hata hivyo, wakuu wa nchi hizo, hawajatoa msimamo thabiti uliohimizwa na wanamazingira, ukitaka nchi wanachama kuunga mkono mkakati wa Brazil wa kumaliza ukataji miti kinyume cha sheria ifikapo mwaka 2030 na ahadi ya Colombia ya kuacha kuchimba mafuta ndani ya msitu huo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.