Pata taarifa kuu

Hatua mpya dhidi ya uchafuzi wa hewa unaosababishwa na magari nchini Marekani

Mpango wa serikali ya Marekani una lengo la wazi kabisa: kuhakikisha kwamba theluthi mbili ya magari yanayouzwa nchini humo mwaka 2032 ni ya umeme.

Magari yalivyonasa kwenye foleni kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani mjini Tijuana, katika jimbo la Baja California, Mexico, tarehe 8 Novemba 2021.
Magari yalivyonasa kwenye foleni kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani mjini Tijuana, katika jimbo la Baja California, Mexico, tarehe 8 Novemba 2021. © AFP / Guillermo Arias
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Kulinda Mazingira la Marekani (EPA) lilipendekeza Jumatano, Aprili 12 kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafu kutoka kwa magari mapya. Lengo ni kupunguza wastani wa uchafuzi wa mazingira kwa 13%. Ni pendekezo linalohitajika zaidi hadi sasa nchini Marekani.

Ili kufikia hili, makampuni ya kutengeneza magari yanapaswa kinadharia kuzalisha 67% ya magari ya umeme ifikapo mwaka 2032. Takwimu muhimu wakati 6% pekee ya magari ya Marekani yaliyouzwa mwaka jana yalikuwa ya umeme.

Utawala wa Marekani unataka kupunguza hatua kwa hatua kiasi cha hewa chafuzi inayozalishwa. Inabakia kwa makampuni ya kutengeneza magari kuchagua kati ya teknolojia kadhaa: kupunguza magari yao, kuboresha injini zao au hata kubadilisha vichujio vya chembe.

Ikiwa sheria mpya zitazingatiwa, uzalishaji wa CO2 unaweza kupunguzwa kwa karibu tani bilioni 10 hadi mwaka 2055. Kwa upande wa wanamazingira wanasema, hii pia itapunguza gharama za mafuta na uagizaji wa mafuta.

Hata hivyo, matatizo kadhaa yanaonekana: kiasi kilichopunguzwa cha malighafi inayopatikana kama vile lithiamu au idadi ndogo ya vituo vya kuchaji. Lakini pia viwango vinavyoweza kubadilika kwa kila mabadiliko ya kisiasa... Jambo ambalo hufanya iwe vigumu kwa makampuni kujipanga kwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.