Pata taarifa kuu

Mkutano maalum wa Umoja wa Mataifa kushughulikia 'shida ya maji safi'

Wakati mkutano maalum kuhusu maji ukifunguliwa Jumatano hii, Machi 22 huko New York, Umoja wa Mataifa unaonya kwamba dunia inapaswa kujiandaa kwa mgogoro wa "maji safi" kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na uchafuzi wa mazingira. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu bilioni 2.3 wanaishi katika nchi zenye shida ya maji na kwamba hilo litazua mivutano isiyoweza kuepukika.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu bilioni mbili bado hawana maji (safi) ya kunywa.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu bilioni mbili bado hawana maji (safi) ya kunywa. AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko New York,

Huu ni mkutano wa kwanza wa aina yake kwa miaka 46! Hata hivyo, hatari ni kubwa. Umoja wa Mataifa tayari ulipaza sauti siku ya Jumanne kwa kuonya kwamba dunia lazima ijiandae kwa "shida ya maji safi" kutokana na ongezeko la joto duniani na uchafuzi wa mazingira. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu bilioni 2.3 wanaishi katika nchi zenye shida ya maji na bilioni mbili hawana maji ya kunywa. Upungufu huu utaleta mvutano kila wakati. Isitoshe ni wazi kuwa nchi hazitafanikiwa kuhalalisha ajenda ya 2030, ambayo ilikuwa ni kuhakikisha upatikanaji wa maji na huduma za vyoo kwa wote.

Kwa hivyo, zaidi ya washiriki 6,500 wanatarajiwa kwa hafla zaidi ya 500 Jumatano na Alhamisi, Machi 22 na 23 huko New York. Na kuunaweza kutarajia ahadi madhubuti. Kwa sababu hata kama hakuna makubaliano ya jumla ya kisiasa yanayotarajiwa, Umoja wa Mataifa utazitaka nchi kujitolea katika siku hizi mbili katika nyanja kadhaa: usafi wa mazingira, kustahimili mafuriko na ukame, maendeleo endelevu. Pia kujitolea kufanya utafiti wa bajeti kuhusu maji.

Pia ni fursa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimazingira kuweka shinikizo kwa nchi: Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) utaziomba uwekezaji zaidi katika mifumo ya ikolojia ya maji safi, kwa mfano. Taasisi ya Rasilimali Duniani inatetea usimamizi mpya wa maji, unaokubalika na mabadiliko ya Tabia nchi na inasisitiza kwamba kupata maji kwa ajili ya jamii zetu kufikia 2030 utagharimu zaidi ya 1% ya Pato la Taifa la dunia, na faida kubwa ya uwekezaji: ukuaji zaidi, kuongezeka kwa uzalishaji wa kilimo, na kuboresha maisha ya jamii maskini.

Barani Afrika, asilimia 90 ya rasilimali za maji zinavuka mipaka

Ili kupunguza mvutano unaohusiana na uhaba wa maji, moja ya mhimili ambao Umoja wa Mataifa unafanyia kazi ni kushinikiza ushirikiano mkubwa wa kuvuka mpaka katika kugawana maji. Kwa hili, inategemea nguzo: Mkataba wa Maji wa 1992. Kimsingi, ilikuwa mkataba kati ya nchi za Ulaya ili kupendekeza wajibu wa nchi zinazoshiriki rasilimali za maji - kugawana mto, bahari au kutegemea bonde moja la chemichemi. Lakini tangu mwaka wa 2016, nchi zote duniani sasa zinaweza kutia saini, imekuwa kama makubaliano ya mfumo, ambayo inaruhusu nchi jirani kuweka kanuni za kuunganisha rasilimali au miundombinu kama vile mabwawa. Baadhi ya nchi 153 kote ulimwenguni yanagawana mabonde ya chemichemi, kwa hivyo mahitaji ni makubwa.

Kuna shauku kubwa kutoka kwa nchi za Kiafrika kwa mkataba huu: Nigeria itatangaza Jumatano kuwa inajiunga nayo. Itakuwa nchi ya saba barani Afrika iliyotia saini. Na hivi karibuni itafuatiwa na Gambia, Côte d’Ivoire, Namibia katika miezi ijayo. DRC, Sierra Leone, Tanzania na Uganda pia zinavutiwa.

Kwa sababu kati ya ongezeko la joto duniani na shinikizo la idadi ya watu, kuna haja ya kweli ya kudhibiti maji haya ya pamoja, hasa kwa vile 90% ya rasilimali za maji barani Afrika zinavuka mipaka. Jinsi gani ya kudhibiti, kwa mfano, kNigeria inatoka kwa wakazi Milioni 200 hadi Milioni 400 ifikapo mwaka 2050, wakati zaidi ya 60% ya wakazi wanaishi katika bonde la chemichemi ya Niger, ambayo inashirikiwa na nchi tisa? Nchi itaweza kutoa tafakari na majirani zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.