Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Marekani: Wahamiaji 39 wafariki katika kisa cha moto katika kituo wanakozuiliwa wahamiaji

Takriban wahamiaji 39 wamefariki na wengine 29 kujeruhiwa katika kisa cha motio uliozuka katika kituo wanakozuiliwa wahamiaji mapema Jumanne walipokuwa wakishikiliwa kaskazini mwa Mexico, huko Ciudad Juárez, mji wa Mexico unaopakana na Marekani, mamlaka imesema.

Mmoja wa waokoaji ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa sababu ya kukosa kibali cha kuzungumza amesema karibu wahamiaji 70, wengi wao wakiwa raia wa Venezuela, walikuwa wakiishi katika eneo hilo.
Mmoja wa waokoaji ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa sababu ya kukosa kibali cha kuzungumza amesema karibu wahamiaji 70, wengi wao wakiwa raia wa Venezuela, walikuwa wakiishi katika eneo hilo. REUTERS - JOSE LUIS GONZALEZ
Matangazo ya kibiashara

Taasisi ya Kitaifa ya Uhamiaji (INM) ambayo inasimamia kituo hiki "inasikitishwa na vifo vya wahamiaji 39 kufikia sasa kufuatia kisa cha moto", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Majeruhi 29 wamelazw, huki wakiwa katika hali mbaya katika hospitali nne, imeongeza INM, ikitangaza utayari wake wa kusaidia familia za waathiriwa.

INM imebainisha kuwaimeanzisha mawasiliano "na mamlaka ya kibalozi ya nchi mbalimbali ili kutekeleza hatua zilizoidhinishwa na utambuzi kamili wa wahamiaji waliofariki".

Moto huo ambao haujawahi kushuhudiwa katika vituo vya wahamiaji nchini humo, ulianza muda mfupi kabla ya saa sita usiku Jumatatu, huku maafisa wa kikosi cha Zima moto na makumi ya magari ya wagonjwa yakitumwa eneo la tukio.

Moo ulianza katika eneo ambalo wageni wasio na hati wanaishi. INM inasema "inafutilia mbali vikali vitendo vilivyotokea katika mkasa huu".

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliweza kuwaona wafanyakazi wa idara ya uchunguzi wakiweka maiti kwenye eneo la kuegesha magari la kituo hicho kabla ya kuchukuliwa kwa utambuzi.

Eneo hilo lilikuwa linalindwa na askari na walinzi wa taifa.

Wahamiaji wengi walikuwa wamehamishiwa katika kituo hiki katika siku za hivi karibuni baada ya kampeni ya serikali za mitaa dhidi ya wachuuzi wa mitaani, ambao ni pamoja na wageni wengi.

Mmoja wa waokoaji ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa sababu ya kukosa kibali cha kuzungumza amesema karibu wahamiaji 70, wengi wao wakiwa raia wa Venezuela, walikuwa wakiishi katika eneo hilo.

Ciudad Juarez, jirani ya El Paso (Texas), ni mojawapo ya miji ya mpakani ambayo wahamiaji wengi wasio na vibali hujaribu kuingia Marekani kutafuta hifadhi.

Tangu 2014, karibu wahamiaji 7,661 wamefariki au kutoweka wakielekea Marekani, kulingana na takwimu za Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Mnamo Machi 13, mamia ya wahamiaji waliochoka, wengi wao wakiwa raia wa Venezuela, walijaribu kuvuka mpaka lakini wakazuiwa kuvuka na maafisa wa Marekani.

Mnamo Juni 27, wahamiaji 56 walipatikana wakiwa wamekosa hewa hadi kufa kwenye trela iliyotelekezwa karibu na San Antonio, Texas.

Watu wapatao 200,000 hujaribu kuvuka mpaka kati ya Mexico na Marekani kila mwezi. Wahamiaji, wakiwa na hamu ya kutoroka umaskini au vurugu katika nchi zao za asili, mara nyingi huchukua hatari kubwa kuingia katika ardhi ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.