Pata taarifa kuu

Marekani: Mahakama ya Juu zaidi yashikilia hatua ya kiafya kuzuia wahamiaji kwenye mpaka

Nchini Marekani, Mahakama ya Juu imeamua kudumisha neno maarufu la "Title 42", hatua inayowezesha kufukuzwa kwa wahamiaji wanaotarajiwa, hata wale wanaotafuta hifadhi. Pamoja na hatua hii, vita vya kisheria kati ya utawala wa Biden na majimbo yanayotawaliwa na magavana kutoka chama cha Republican vinaendelea.

Wahamiaji wakikusanyika kwenye mpaka wa Mexico na Marekani kwenye Mto Rio Grande, wakipewa ulinzi na kikosi cha Walinzi wa kitaifa wa Texas, Desemba 20, 2022.
Wahamiaji wakikusanyika kwenye mpaka wa Mexico na Marekani kwenye Mto Rio Grande, wakipewa ulinzi na kikosi cha Walinzi wa kitaifa wa Texas, Desemba 20, 2022. © Morgan Lee / AP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo iliwekwa na Donald Trump mnamo mwezi Machi 2020 kupambana na janga la UVIKO-19. Utawala wa Biden sasa unataka kuifuta, isipokuwa kwamba majimbo kadhaa yanayotawaliwa na magavana kutoka chama cha Republican nchini, 19 kwa jumla, wanaamini kuwa isababisha mzozo mkubwa zaidi kwenye mpaka, na kuwasili nchini Marekani kwa wahamiaji wengi.

Mahakama ya Juu inapaswa kutoa uamuzi katika miezi ijayo, lakini wakati huo huo, majaji watano kati ya tisa wameamua kuacha hatua hiyo iendelea kutumika. Mmoja wa majaji wahafidhina, Neil Gorsuch, hata hivyo alipiga kura na wenzake kwa kueleza kwamba "Title 42 " iliwekwa ili kukabiliana na mgogoro wa afya, na mgogoro wa uhamiaji sio mgogoro wa afya".

Kwa upande wake, Seneta kutoka chama cha Republican kutoka Louisiana, Bill Cassidy, amebaini kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa kutangaza: "Nimefurahi kuona uingiliaji huu wa Mahakama ya Juu kuhifadhi [Title 42], lakini tunahitaji suluhisho la kudumu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.