Pata taarifa kuu

Maelfu ya watoto wahamiaji watumiwa katika viwanda nchini Marekani

Nchini Marekani, ufichuzi wa gazeti la New York Times juu ya utumiaji wa watoto wadogo, hasa kutoka Amrika ya Kusini, katika viwanda vikubwa vinavyofanyia kazi bidhaa maarufu umezua taharuki. VMashirika ya kutetea haki za wahamiaji na wanasiasa wengi wanalaani tabia hiyo ambayo wanaeleza isiyokubalika.

Maelfu ya watoto kutoka Amerika Kusini huwasili Marekani kila mwaka. Wengi wao hufika bila wazazi.
Maelfu ya watoto kutoka Amerika Kusini huwasili Marekani kila mwaka. Wengi wao hufika bila wazazi. REUTERS - JOSE LUIS GONZALEZ
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la New York Timesndilo  ambalo lilichunguza watoto hawa wahamiaji waliolazimishwa kufanya kazi katika viwanda, vichinjio, maeneo ya ujenzi, mashamba ya kilimo, hasa nyakati nyingine usiku. Watoto hao wana umri wa miaka 15, 16 na hata, baadhi ya wengine, hawana umri wa miaka 12 kulingana na mahojiano zaidi ya mia moja yaliyofanywa. Makala hiyo inaelezea mazingira magumu sana ya kazi na wachimbaji madini ambao wanajikuta wamenaswa katika mfumo wa uchimbaji unaokiuka kabisa sheria za ajira ya watoto nchini Marekani.

Idadi kubwa ya watoto wanatoka nchi za Amerika ya Kati na waliwasili peke yao nchini Marekani. Wanatakiwa kwenda kuishi na familia zao au kuwekwa katika familia zitazowapokea na kuishi nao. Kimsingi, wanaenda shule, lakini wengine wanadaiwa pesa na wasafirishaji waliowavusha mpaka. Wengine wanasukumwa kufanya kazi na watu wanaowapokea. Na kisha kuna wale ambao wanataka tu kutuma pesa kwa familia zao ambao hawajaweza kuvuka mpaka.

Ongezeko kubwa la ajira haramu kwa watoto

Ufichuzi ho unatoa tahadhari nyingi kwa sababu unaonyesha kwamba idadi kubwa ya watoto wasio na wazazi wanahusika. Wahamiaji wasio na umri mdogo kulazimishwa kufanya kazi ni ukweli katika angalau majimbo ishirini ya Marekani. Na katika viwanda vinavyofanya kazi kwa makampuni na chapa zinazojulikana kama vile maduka makubwa ya Whole Foods, Walmart, Target, General Motors na Ben na Jerry's. Hii inaonyesha kiasi gani tabia hiyo imekuwa sugu.

Idadi ya watoto walioajiriwa kinyume cha sheria nchini Marekani imeongezeka kwa 69% tangu mwaka 2018. Kulingana na Gazeti la New York Times, hii inahusishwa kwa sehemu na kuongezeka kwa idadi ya watoto wasio na hati wanaowasili kwenye mpaka wa kusini bila kuandamana na wazazi wao. Kulikuwa na zaidi ya watu 130,000 mwaka jana, mara tatu zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Ukiukaji wa wazi wa sheria za kazi

Muda mfupi baada ya kuchapishwa kwa uchunguzi wa Hannah Dreier wa New York Times, utawala wa Biden uliahidi kuimarisha udhibiti ili kuwalinda watoto hawa. Jibu lililoonekana kutotosha kwa baadhi ya viongozi waliochaguliwa. Kundi la Wanademokrasia walituma barua kwa utawala wa Biden wakitaka maelezo ifikapo Aprili 1. Wanatoa wito kwa udhibiti mkali zaidi katika viwanda na maeneo ya ujenzi. Pia wanataka udhibiti mkali juu ya familia za zinazowalea  ambazo watoto hawa wanawekwa ili kuhakikisha kwamba hawatanyanyaswa.

Katika mwaka uliopita wa fedha nchini Marekani, Wizara ya Kazi ilibainisha makampuni 835 ambayo yaliajiri watoto 3,800 kinyume na sheria na kuona ongezeko la 26% la watoto walioajiriwa hasa katika nafasi za hatari.

Mashirika yanayosimamia kazi yalijitetea kwa kueleza kwamba kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaoingia Marekani pekee, walijaribu kupendelea mwendo kasi, wakati mwingine kwa hasara ya ukaguzi wa lazima, ili wasiwaache watoto katika vituo vilivyojaa watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.